ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 6, 2017

MANDELA NI NEMBO YA MAPAMBANO DHIDI YA UBAGUZI WA RANGI ASEMA MWAKILISHI WA IRAN UN.

Ghulam Ali Khosro.
Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemtaja hayati mzee Nelson Mandela kuwa nembo ya mapambano dhidi ya ukandamizaji na ubaguzi wa rangi.

Mwakilishi huyo wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameyasema hayo baada ya kutembelea maonyesho ya picha za Nelson Mandela yaliyotayarishwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mwanasanaa wa Kiirani kwa jina la Maitham Shah Babai. 

 Mwanasanaa huyo wa Kiirani ambaye ni mpiga picha, mtengeneza filamu na mwandishi kijana anafanya maonyesho ya picha ya hayati mzee Nelson Mandela kiongozi wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini tangu tarehe 3 hadi 6 mwezi huu wa Januari. 

Maonyesho hayo yamefanyika katika moja ya kumbi za kijamii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Ghulam Ali Khosro  Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa jana alipongeza jitihada za msanii huyo kijana wa Iran katika siku ya pili ya kufanyika maonyesho hayo huko New York. 
Mzee Nelson Mandela (kushoto), enzi za uhai wake

Khosro baadaye aliandika katika kitabu cha kumbukumbu baada ya kutembelea maonyesho hayo ya picha za mzee Nelson Mandela kuwa, " Nelson Mandela shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, mapambano ya mshikamamo wa kitaifa na kukabiliana na ukandamizaji".


 Nelson Mandela kiongozi aliyeongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini (Apartheid) na rais wa zamani wa nchi hiyo aliaga dunia tarehe 5 Disemba mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 95.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.