ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 21, 2017

MAELFU WAANDAMANA MJINI WASHINGTON KUPINGA URAIS WA DONALD TRUMP.


MAELFU ya wananchi wa Marekani wanaendelea kumiminika mjini Washington kupaza sauti zao wakieleza hasira na wasiwasi wao kuhusu urais wa Donald Trump, siku moja tu baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa 45 wa Marekani.
Maandamano ya Wanawake mjini Washington ambayo watayarishaji wake wanasema yatawakutanisha pamoja malaki ya watu, yana lengo ya kuwazindua Wamarekani kuhusu haki za wanawake na haki nyingine za kiraia ambazo Wamarekani wengi wana wasiwasi kwamba zinatishiwa na rais mpya wa nchi hiyo.
Trump amewakasirisha watu wengi ndani na nje ya Marekani kwa kukariri matamshi yanayowashushia hadhi wanawake, Waislamu na wahamiaji wakati wa kampeni zake za urais.

Wamarekani waandamana dhidi ya Rais Donald Trump.
Maandamano ya Jumamosi ya Wanawake ambayo yalianza kwa wito uliotolewa na bibi wa Hawai katika mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya ushindi wa Donald Trump mwezi Novemba mwaka uliopita, yanahesabiwa kuwa maandamano makubwa zaidi ya kisiasa kuwahi kushuhudiwa katika mji mkuu wa Marekani.
Wapinzani wa Rais Donald Trump wa Marekani walikuwa wakiendelea kumiminika mjini Washington kwa mabasi wakitokea katika miji na maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Richmond, Crystal Hoyt, anasema leo Wamarekani watashuhudia moja kati ya maandamano makubwa na muhimu zaidi ya kupigania uadilifu wa kijamii katika historia ya miaka 240 ya Marekani. Profesa Crystal Hoyt ameongea kuwa, Trump ametumia siasa za kuchochea hofu, ubaguzi wa kijinsia na chuki dhidi ya wageni na wahamiaji kwa ajili ya maslahi ya kisiasa.

Maandamano ya Washington.
Maandamano ya leo mjini Washington yanafanyika siku moja baada ya sherehe za jana za kuapishwa Rais mpya wa Marekani zilizoandamana na maandamano na ghasia ambazo ni kielelezo cha mgawanyiko mkubwa unaotawala jamii ya Marekani kutokana na siasa za kibaguzi za rais mpya wa nchi hiyo.
Polisi ya Washington imetangaza kuwa imewatia nguvuni waandamanaji wasiopungua 217 katika maandamano na machafuko ya jana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.