ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 29, 2017

BREAKING NEWS: HATIMAYE WATU 15 WALIOFUKIWA GEITA WATOLEWA WAKIWA WAZIMA.

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, hatimaye wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ uliopo Nyarugusu, wilayani Geita mkoani Geita wameokolewa wote wakiwa hai. 

Tangu usiku wa saa 7 kuamkia Alhamisi wakichimbaji hao wamekuwa chini ardhini wakishindwa kujua nini hatma yao baada ya udongo kutitia na kufunika sehemu ya tundu ambalo ndilo mlango wa kutokea shimoni humo.


KWA UFUPI
Mchana na usiku juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika kutoka kwa wataalamu wa uokozi kutoka migodi jirani na wengine kutoka serikalini na hatimaye jana mwanga wa matumaini ukaanza kuonekana mara baada ya watu hao kugonga bomba linalosafirisha hewa na kishindo kusikika juu.

Walishusha tochi na radio kupitia bomba hilo, kamba ikarudi tupu hii ikimaanisha kuwa vimepokelewa lakini mawasiliano yakakosekana. Kisha wakashusha barua, kalamu na karatasi vyote vikapokelewa.

Barua waliijibu wakisema kuwa wote 15 ni wazima isipokuwa mmoja amechomwa na msumali na wakaandika majina yao,wakihitaji chakula.

Team ya madaktari ilitoa angalizo kwamba wasishushiwe chakula bali dripu tu kwani wanatakiwa kunywa maji tu kwamaana hawajala siku 2.

Zikashushwa dripu maalum za maji kupitia bomba hilo naam ndizo zinasadikika kuwasogeza. 

Sehemu ya Askari Polisi na wa Kikosi cha uokoaji wakiendelea na zoezi la uokozi kwa waathirika wa tukio hilo, asubuhi ya leo.


Hivi ndivyo zoezi la uokoaji kwa ndugu zetu hao lilizovyofanikiwa kwa jitihada za vikosi vya usalama na uokoaji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.