ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 29, 2017

HUJUMA ZA UCHOMAJI MOTO MISIKITI ZAENDELEA NCHINI MAREKANI.


KATIKA muendelezo wa sera zinazotajwa ni chuki dhidi ya Uislamu na hujuma zinazolenga misikiti nchini Marekani, vyombo vya usalama vya nchi hiyo vimeripoti kuwa msikiti mwingine mmoja umechomwa moto katika jimbo la Texas.
Kanali ya televisheni ya Fox News imezinukuu duru za usalama kuwa moto umeteketeza na kuharibu sehemu kubwa ya msikiti huo ulioko kwenye mji wa Victoria katika jimbo la Texas. Kwa mujibu wa ripoti hiyo chanzo cha moto huo, ambao hata hivyo haukusababisha maafa kwa mtu yeyote, bado hakijajulikana.
Shambulio dhidi ya msikiti huo ni hujuma ya pili kulenga msikiti katika jimbo hilo katika kipindi cha mwezi huu wa Januari.

Hali ya msikiti wa kituo cha Kiislamu cha Victoria baada ya kuchomwa moto.
Tarehe 7 mwezi huu msikiti uliokuwa ukiendelea kujengwa karibu na eneo la Mto Travis katika mji wa Austin ulichomwa moto na kuteketezwa kikamilifu.
Miaka michache nyuma, kituo cha Kiislamu cha Victoria kinachojumuisha msikiti huo wa Texas kilishambuliwa mara kadhaa na watu wenye misimamo ya kibaguzi.
Maafisa wa Marekani wamekiri kuwa misikiti kadhaa ya maeneo tofauti ya nchi hiyo imeshambuliwa katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.
Baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa hotuba na matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu yanayotolewa na rais mpya wa Marekani Donald Trump yamesababisha kushamiri misimamo ya kufurutu mpaka nchini humo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.