ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 16, 2017

HATIMAYE AHADI YA MAJI KWA JIMBO LA KISESA YATIMIA.

NA ZEPHANIA MANDIA.

 ZAIDI ya wananchi 2800 wa vijiji viwili vya Sakasaka na Bulyanduru wilayani Meatu vilivyopo katika Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu wameanza kunufaika na mradi wa maji safi uliotekelezwa na Serikali, ikiwa ni kuondokana na adha waliyokuwa wakiipata wananchi hao hususani akina mama ambao wamekuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata maji katika maaeneo ya mbali huku wakiacha shughuli zao za kilimo ambazo huwaingizia kipato hali ambayo ilikuwa ikipelekea kuyumba kwa uchumi.

Mradi huo wa maji ulioghalimu zaidi milioni 235  utakuwa na uwezo wa kusambaza maji katika vituo 64 hali ambayo itapelekea wananchi kupata maji kwa uraisi kuliko hapo awali ambapo walikuwa wakinunua ndoo moja ya lita 20 kwa shilingi 500, sasa wamekuwa wakinunua ndoo  moja kwa shillingi 50.
Akizungumza katika makabidhiano ya muradi huo naibu waziri wa Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, amewataka wananchi hao kuhakikisha wanatunza miradi ya maendeleo wanayoletewa ili kuweza uwahudumia kwa muda murefu.

Hayo yalisemwa jana na  Mbunge wa jimbo la Mwandoe Luhaga Mpina, wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliopo katika kijiji cha Bulyandulu kata ya Sakasaka Mkoani Simiyu wenye dhamani ya shilingi milioni 235, alisema mradi huo Hata hivyo Mpina, aliwahakikishia wananchi wake kuwa vitongoji ambavyo havijafikiwa naMradi huo atafanya kila hali wanachiwake wapate maji safi.

 Katika kuhakikisha juhudi za hizo zinafanyika, amemtaka mkandarasi kuendelea kutandaza bomba za maji katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mradi huo ili maji yaweze kutoka kila kila kijiji.

 Pia aliwataka wananchi kulipia bili za maji kwa wakati na kama mtu akishindwa kulipia bili akatiwe maji kwasababu fedha zinazokusanywa ni kwaajili ya kukidhi mahitaji ya kuhudumia mradi huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.