ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 17, 2016

MAHAKAMA YATUPA PINGAMIZI LA SERIKALI KATIKA KESI YA MBUNGE LEMA

RUSHA: Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali pingamizi la mawakili wa serikali ilizoweka dhidi ya taarifa ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godblees Lema.
Jaji Modesta Opiyo wa mahakama kuu kanda ya Arusha alisema katika maamuzi yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi walifuata taratibu zote  katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa mahakamani.

Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shedrack Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha hoja zao katika kiapo na hati ya dharura.

Akizungumza baada ya kukubaliwa na Jaji ,wakili Mfinanga alimtaka Jaji huyo kusikiliza rufaa hiyo kwani kuchelewa siyo sababu ya msingi sana kwa mujibu wa sheria na kunukuu kesi mbalimbali zilizochelewa kukatiwa rufaa kwa siku nyingi na kudai kuwa mahakama ya rufaa ilizikubali na kuzitolea maamuzi.

Mfinanga alisema na kumwomba Jaji kusikiliza rufaa yao kwa sababu ni ya msingi na kamwe haiwezi kuvunja sheria ya makosa ya jinai iliyowekwa kwa mujibu wa sheria.

Mawakili wa serikali wakiongozwa na Wakili Mfawidhi Materius Marandu, Hashim Ngole na Elizabert Swai walipinga vikali kukubaliwa kwa rufaa hiyo kwa madai kuwa Jaji Msengi alitupilia mbali na kurudia kuikubali ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za makosa ya Jinai.

Baada ya malumbano hayo yaliyochukuwa zaidi ya masaa 5  Jaji Opiyo alisema kuwa uamuzi wa kuikubali ama kuikataa rufaa hiyo atautoa Desemba 20 mwaka huu majira ya saa 6 mchana katika mahakama hiyo.

Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi aliyosomewa katika mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka huu Mkoani Dodoama kwa kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika kata mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi kwa wananchi waliomchagua kuwa Rais wa nchi.

MBUNGE SUGU APATA AJALI, MTOTO AFARIKI KWENYE AJALI HIYO.

Taarifa zilizoripotiwa na kituo cha runinga cha ITV leo December 17 2016 zinasema kuwa mbunge wa Mbeya mjini ‘CHADEMA’, Joseph Mbilinyi amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Iyunga jijini Mbeya baada ya gari lake kufeli break na kumgonga mtoto  ’15’ ambaye amefariki wakati akipelekwa hospitali.
Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa askari polisi wanne wamejeruhiwa baada ya kupata ajali wakati wakielekea kwenye ajali hiyo aliyopata mbunge Joseph Mbilinyi  ‘sugu’

Gari hilo lilikuwa  linaendeshwa na dereva wake, Gabriel Andrew (43) ambaye anashikiliwa na polisi.

RAIS MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI DKT MWELE MALECHELA.

Rais John Magufuli atengua uteuzi wa mkurugenzi wa mkuu wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Dkt. Mwele Malecela.

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MWEKA HAZINA BAHI.


SIMU.tv: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amsimamisha kazi mweka hazina mwaka hazina ya wilaya ya Bahi kwa ubadhilifu wa fedha za umma.

WAZIRI WA UJENZI MGUU KWA MGUU, SHINGO KWA SHINGO NA WAKANDARASI.


Waziri wa Ujenzi Prof.Makame Mbarawa awataka makandarasi nchini kumaliza kazi zao kwa wakati. 

Friday, December 16, 2016

MWENYE NYUMBA WA MSAIDIZI WA MBOWE AELEZA ILIVYOKUWA.

Dar es Salaam. Mmiliki wa nyumba anayoishi kada wa Chadema, Ben Saanane aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha mwezi mmoja uliopita, Evance Mrosso amesema waligundua kuwa amepotea baada ya siku nne kupita bila kuonekana.
Mrosso aliyekuwa akiishi na Saanane maeneo ya Tabata Dampo, jana alifunguka kuwa haikuwa kawaida yake kukaa kimya kwa muda mrefu kwani ni mtu wa mawasiliano kwa ndugu zake, marafiki na majirani.

“Saanane ni mtu wa kutoka asubuhi na kurudi usiku na inaweza ikapita siku mbili tusionane kutokana na mwingiliano wa shughuli zangu na zake, lakini tunawasiliana kwa simu, ” alisema Mrosso.

Hata hivyo, Mrosso alisema hali ilikuwa tofauti baada ya kupita siku hizo nne ndipo aliamua kuwauliza jirani zake kama wamemuona na walimjibu kuwa hawajamwona.

“Nimeishi na Saanane kwa muda wa miaka mitano.Mara ya mwisho tulionana na kuwasiliana Novemba 12, wakati wenzangu tunaoishi nao walimuona kuanzia tarehe hiyo hadi 14, hata wao walishangaa kutomuona kwa sababu siyo kawaida yake,” alidai Mrosso.

Alisema baada ya kujibiwa hivyo, alichukua uamuzi wa kumtafuta kumpigia simu katika namba zake mbili alizokuwa akitumia lakini hazikupatikana.

Alisema baadaye aliamua kumpigia simu mmoja wa dada zake anayeishi Mbeya ili kumweleza suala hilo na kama aliwasiliana naye hivi karibuni.

“Dada yake akaniambia hawajawasiliana na Saanane kwa muda sasa. Hivyo alinishauri nitoea taarifa polisi. Lakini kabla ya kwenda polisi, nilienda ofisini kwake Chadema (Kinondoni) kumuulizia, nilimkuta mlinzi akanieleza kuwa hajaonekana kwa siku kadhaa ofisini hapo,” alidai Mrosso.

Juzi, Mwanasheria wa Chadema, Tundu lissu aliitaka Serikali kueleza kama inamshikilia kada huyo ambaye alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe.

Sanjari na hilo, Lissu aliitaka Serikali kufuatilia ujumbe wa vitisho aliowahi kutumiwa Saanane kupitia simu yake ya mkononi na mtu ambaye bado hajafahamika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni alisema polisi bado inaendelea na upelelezi.

“Taarifa zilizopo ni za kipelelezi hatuwezi tukaziweka hadharani, wakati uchunguzi wa tukio hili ukiendelea,” alisema Kamanda Hamduni.

CHANGAMOTO YA MAJISAFI, LESENI, VIBALI VYA USAFIRISHAJI NA UMEME VYACHELEWESHA DHAMIRA YA SERIKALI.

Na Peter Fabian, MWANZA.

KAMPUNI mbalimbali za Uwekezaji zilizojitokeza Mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchini zimedai kukabiliwa na changamoto za upatikanaji wa majisafi, leseni, vibali vya usafirishaji nje ya nchi na umeme katika maeneo wanayotaka kujenga viwanda hivyo kuchelewesha dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.

Changamoto hiyo imetolewa na juzi na baadhi ya Kampuni zilizojitokeza kuwekeza viwanda mbalimbali katika mikoa ya Kanda ya Ziwa zilizofika katika Ofisi za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) zilizopo jijini Dar es salaam na Kanda ya Ziwa  ili kupata taratibu na ushauri kabla ya kuanza kujenga viwanda kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kituo cha TIC nchini , Clifford Tandari aliwaeleza baadhi ya wawekezaji waliombioni kujenga viwanda katika mikoa ya Mwanza na Simiyu kuwa dhamira ya serikali ya awamu ya tano ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

Tandari alieleza kwamba amezipokea changamoto hizo za Kampuni ambazo bila kutafutiwa ufumbuzi wa haraka zinaweza kuwakimbiza kna kuacha kuwekeza viwanda katika maeneo mbalimbali nchini hivyo kuahidi TIC kushirikiana na Wizara, Taasisi na Mamlaka zingine za serikali kuhakikisha ucheleweshaji huo unamalizika haraka na kampuni zote zinajenga viwanda haraka kama ilivyokusudiwa na serikali .

“TIC tumejipanga kushughulikia changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka zinazofikisha kwetu na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuondoa urasimu na ucheleweshaji unaoweza kuwakwamisha wawekezaji wa viwanda, hoteli na utoaji huduma nyingine za kijamii,”alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba adhima ya serikali ya awamu ya tano ni Tanzania ya Viwanda  vikubwa, vyakati na vidogo kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo tangu Rais Dk John Magufuli aingie madarakani mwezi Novemba mwaka 2015 hadi sasa Desemba 2016 tayari Kamupini 136 zimejitokeza kuwekeza viwanda.

“Kituo cha TIC kimeisha fikiwa na wawekezaji wa kampuni 136 za ndani na mataifa nje yanayotaka kuwekeza kwa kujenga viwanda vikubwa, vyakati na vidogo hapa inchi nasi TIC tumewahakikishia kuwa tutahakikisha vikwazo na changamoto ikiwemo upatikanaji wa maeneo ya uwekezaji havitakuwa kikwazo kwa,”Alisema.

Tandari ametoa wito kwa Kampuni mbalimbali zinazokusudia kuwekeza kufika katika Kituo cha TIC ili kuwezesha kupata ushauri na kuwasaidia kukamilisha taratibu za kisheria za kuwekeza ili wanapopata matatizo waweze kusaidiwa kwa kuwa wanakuwa na mikataba ya kitaifa na kimataifa ya sheria ya uwekezaji.

Naye Meneja wa TIC Kanda ya Ziwa, Fanuel Lukwalo aliwatambulisha wamiliki na wawakilishi wa Kampuni  za Nyanza Bottiling Ltd (Mwanza) inayotaka kupanua kiwanda kuongeza uzalishaji wa vinywaji baridi, Mwanza Hollidring Ltd inayotaka kujenga kiwanda cha saruji eneo la Nyamatembe lililopo wilayani Busega Mkoa wa Simiyu.

Lukwalo aliwatambulisha Kampuni ya Premidis Ltd iliyo mbioni kujenga kiwanda cha vinywaji vya vileo eneo la Nyakati Wilaya ya Nyamagana na Kampuni ya MRS Wang ya nchini China cha kukausha mabondo ya samaki eneo la Pasiansi Wilaya ya Ilemela, Kampuni ya CMG Ltd ya jijini Mwanza inayojenga kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za saruji .

Thursday, December 15, 2016

KAMPUNI YA PENNYROYAL GIBRALTAL LIMITED YATILIANA SAINI NA KAMPUNI YA MCC OVERSEAS UJENZI WA MRADI WA HOTELI NA NYUMBA KATIKA KIJIJI CHA UTALII MATEMWE ZANZIBAR.

 
 
Mkurugenzi wa Mradi wa Ujenzi Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar Pennyroyal Gibraltar Limited Zanzibar Amber Resort Mr. Saleh Mohammed Said akizungumza kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya utilianaji wa Saini ya Ujenzi wa Mradi huo na Kampuni ya MCC Overseas Ltd ya China, hafla hiyo ya utianaji wa saini hyo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Mradi wa Ujenzi Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar Pennyroyal Gibraltar Limited Zanzibar Amber Resort Mr. Saleh Mohammed Said akizungumza kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya utilianaji wa Saini ya Ujenzi wa Mradi huo na Kampuni ya MCC Overseas Ltd ya China, hafla hiyo ya utianaji wa saini hyo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar.kulia Mkurugenzi Mkuu wa Pennyroyal Gibraltar Limited Mr Brian Thomson akiwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya MCC Overseas Limited ya China Mr Leo Zou.wakiwa katika ukumbi wa hafla hiyo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Limited "Zanzibar Amber Resort" Mr Brian Thomson na kulia Mwenyekiti wa Kampuni ya MCC Overseas Limited ya China Mr. Leo Zou, wakitiliana saini ya ujenzi wa Mradi huo wa Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja. akishuhudia utilianaji wa saini hiyo katikati Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Mr. Khamis Mussa.    
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Limited "Zanzibar Amber Resort" Mr Brian Thomson na kulia Mwenyekiti wa Kampuni ya MCC Overseas Limited ya China Mr. Leo Zou, wakibalishano mikatabaa hiyo baada ya kusaini.ujenzi wa Mradi huo wa Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja. akishuhudia utilianaji wa saini hiyo katikati Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Mr. Khamis Mussa. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Limited "Zanzibar Amber Resort" Mr Brian Thomson, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Kampuni ya MCC Overseas Limited ya China Mr. Leo Zou, akizunguma baada ya hafla ya utilianaji wa saini ujenzi wa mradi wa Kijiji cha Utalii cha Matemwe Zanzibar  
Wageni waalikwa wakifuatila hafla hiyo ya utilianaji wa saini baina ya Pennyroyal Gibraltar Limited na MCC Overseas Limited ya China itakayojenga majengo ya Mradi huo huko Matemwe Zanzibar. Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wawakilishi wa Kampuni ya MCC Overseas limited ya China wakifuatilia hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa akizungumza baada ya hafla hiyo utilianaji wa saini baina ya Kampuni ya Pennyroyal na MCC Overseas.  
Waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa akimsikiliza Mwenyekiti wa MCC Overseas Mr. Leon Zou, wakibadilishana mawazo baada ya hafla hiyo.
Muwekezaji wa Mradi wa Pennyroyal Zanzibar Mr Brian Thomson akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa, baada ya kumalizika kwa hafla ya utilianaji wa saini. 














Wafanyakazi wa Pennyroyal wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaslizika kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu Pennyroyal Mr Brian akibadilisha mawazo na wageni wakati wakati wa kupata viburudisho katika viwanja vya hoteli hiyo.
Wageni waalikwa wakiwa katika viwanja vya hoteli Park Hyyat wakipata vitafunio baada ya hafla hiyo.
Kikundi cha Taarab cha Dulla Ganuni kikitoa burudani wakati wa hafla hiyo. katika viwanja vya Park Hyyat Shangani Zanzibar 

Imeandaliwa na OthmanMapara.blog.
Zanzinews.com
othmanmaulid@gmai.com
0777 424152 0715424152

UMOJA WA WAMILIKI WA DALADALA WAMLILIA WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA KUSIKIA KILIO CHAO

 Daladala zinazo fanya safari kati ya Tegeta Nyuki zikiwa zimesongamana katika Kituo cha  Daladala  nje ya geti Kuu la Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam juzi baada ya kupangiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Nchikavu na Majini (SUMATRA)  yawe yanashusha na kupakia hapo na kusababisha adha kubwa ya abiria na madereva hao walitii nakuyapeleka magari yao Muhimbili kama walivyo elekezwa na (SUMATRA)  nakumfanya Diwani wa Kata ya Upanga Magharibi, Adnan Kondo kuwaamuru waondoke na warudi walikotoka 
 Hapa abiria wakishuka katika mabasi hayo ya Daladala juzi. 
(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
  Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter Mashishanga (kulia)  akizungumza jambo Dar es Salaam jana wakati alipofanya ziara ya kutembelea baadhi ya vituo vya mabasi vya Muhimbili, Feri na Gegerezani akiwa amwongozana na Viongazi mbalimbali wa SUMATRA, Wamiliki wa Mabasi hayo, Madereva na Wenyeviti na makatibu hasa wanjia ya Tageta kujionea hali halisi na changamoto ili waweze kuzitolea majawabu
 Ofisa leseni na Udhibiti Usafiri wa barabara Mkoa wa Dar es Salaam, Bernard  akilipiga picha Gari  Moja  lilofika kwa majaribio katika Kituo cha Mabasi cha Muhimbili
 Kaimu Katibu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala (katikati aliyevaa miwani)  akizungumza jambo wakati wa Ziara ya Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter Mashishanga kutembelea maeneo mbalimbali ya vituo iliwemo Kituo cha Daladala cha Muhimbili ambapo alianzia hapo na kutembelea Feri na Gerezani Dar es Salaam jana
  Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter Mashishanga (kulia) akizungumza jambo wakati walipofika katika Kituo cha Mabasi cha Feri kwa lengo la kujionea changamoto mbalimbali 

 Kituo cha Gerezani Daladala Zikiwa zimesongamana huku wakiwa wanapakia Abiria kwa zamu
Mwenyekiti wa Daladala Zinazofanya Safari ya Tegeta Nyuki (Gosbart mushaka) akizungumza jambo wakati Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter Mashishanga kufika katika Kituo cha Gerezani na Timu yake kujionea hali halisi zilizopo kituoni hapo na aweze kujadiliana na viongozi mbalimbali na kulipatia jawabu swala la Daladala za Tegeta Nyuki ambazo awali zilikuwa zikipaki Kariakoo Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog