ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 19, 2016

CHADEMA MGUU KWA MGUU MAHAKAMANI.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hakikubaliani na agizo la serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Jiji la kuwataka wanaotakiwa kuhudhuria kwenye kikao cha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam wawe ni wajumbe pekee watakaopiga kura.

Chama hicho kimekataa agizo hilo na badala yake kinataka wananchi wote wa jiji la Dar es salaam wahudhurie katika kikao hicho.

Msimamo huo wa Chadema unapingana na barua ya wito wa mkutano wa uchaguzi huo iliyoandikwa Machi 15, 2016 na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sarah Yohana, iliyosema kuwa watakaoruhusiwa kuingia katika viwanja hivyo ni wajumbe pekee ambao ni wapigakura.
Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Mwita Waitara alisema sheria na kanuni zinaruhusu wananchi kushiriki kikao hicho cha wazi, hivyo Yohana hana mamlaka ya kuwazuia.

“Sisi tunafuata sheria na kanuni, barua ya mkurugenzi inaeleza kinyume cha utaratibu,” alisema.

Alisema kufuatia hali hiyo, Ukawa umemwandikia barua Mkurugenzi huyo ya kutokubaliana na matakwa yake ya kuzuia wafuasi wa vyama kuingia ukumbini wakati wa uchaguzi kwani ni uvunjifu wa sheria na kwamba hawatakubali, bali watawapigania na kuhakikisha wananchi wanaingia ukumbini.

Katika hatua nyingine, Waitara alisema CCM kwa sasa  inawaandaa wanachama feki wa CCM wakiongozwa na wakili Elias Nawela kufungua kesi ya madai huku wakitaka wajumbe 9 toka Zanzibar na 11 kutoka mikoa mingine kushiriki uchaguzi wa meya.

Alisema, ili kukabiliana nao, wameamua kuwafuata hukuhuko mahakamani  ambapo tayari wameshatuma maombi ya  kujiunga na kesi hiyo  namba 39  ya  mwaka 2016 huku wakiwa na mawakili wao ambapo inatarajiwa kusomwa Machi 21 mwaka huu katika Mahakama ya Kisutu.

KITWANGA ASEMA PEMBA NI SHWARI, WAZIRI WA KIKWETE KATIKA KASHFA MPYA, LISSU AWA KITUKO AWA KITUKO KAMATI YA BUNGE.


Kitwanga asema Pemba ni shwari, Waziri wa Kikwete katika Kashfa mpya, Lissu awa kituko awa kituko kamati ya bunge.  

CHADEMA yawafuata CCM mahakamani kisa Umeya, Kumekucha Zanzibar, Busu la Papa Fransis lamponya uvimbe mtoto.   

Friday, March 18, 2016

WAMILIKI WASILAHA DAR ES SALAAM WAPEWA SIKU 90 TU.

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wanaomiliki silaha kihalali wametakiwa kwenda vituo vya polisi kuhakiki silaha zao ndani ya siku 90 na wale wanaomiliki silaha hizo bila kibali kuzisalimisha kabla ya operesheni maalum ya kusaka silaha hizo kuanza.

MWENYEKITI UWT MKOA WA DAR ES SALAAM AWANYOSHEA KIDOLE WALIOKISALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Massaburi, akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana, katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Massaburi (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joel Kafuge, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala, Apruna Humba na Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Maliaga.
 Wanawake wa CCM Wilaya ya Ilala wakiwa kwenyev mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Masaburi amesema wanachama wa chama hicho waliokiuchumu wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wasitegemee kupata uongozi wowote ndani ya chama hicho.

Masaburi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukichagua chama hicho na kukipa ushindi ambapo kimeunda Serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.

"Kunawenzetu walitusaliti wakati wa uchaguzi mkuu na kuchangia mkoa wa Dar es Salaam kushindwa kufanya vizuri hali iliyosababisha kuwepo na changamoto hata ya kumpata Meya wenzetu hao tunawafahama na hawatapata nafasi ya kupata nafasi ya uongozi ndani ya chama chetu" alisema Massaburi.

Massaburi alisema ni heri kubakiwa na wanachama wachache waadilifu ndani ya chama kuliko kuwa wengi ambao ni wasaliti na katika jambo hilo ataendelea kulisimamia na kupigania maslahi ya chama ambacho anakitumikia.

Katika hatua nyingine Massaburi aliwataka wana umoja huo kushikamana na kushirikiana na kuhakikisha nguvu yao inaendelea kukipa ushindi chama hicho wa kushika dola kwani jambo hilo linawezekana kwa asilimia 100.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA DUKA LA MSD WILAYANI CHATO


Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Laurean Bwanakunu (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya Waziri Mkuu hajafungua duka la dawa la MSD Wilayani Chato juzi.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim M. Majaliwa (wa tatu kushoto), akizungumza wakati akifungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), Wilayani Chato.


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), la Wilayani Chato duka litakalotoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu alisema duka hilo ni mfano kwa Wilaya nyingine na mikoa,ambapo tayari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa(Tamisemi) mikoa na Wilaya kuanzisha maduka hayo,na kisha MSD itatoa ushauri wa kitaalam.


Bwanakunu alisema kwa kuanza,duka la dawa la Halmashauri ya Chato linaendeshwa na MSD,lakini baada ya muda watalikabidhi kwa Halmashauri ya Chato. 

MAGAZETI YA LEO> WAZIRI MKUU AINGIZWA MKENGE TPA, SEIF ATIBIWA KWA MAMILIONI YA SMZ, CCM YATAHADHARISHWA KUHUSU BALOZI MWAPACHU.

Waziri mkuu  aingizwa mkenge TPA. Seif atibiwa kwa mamilioini ya SMZ.  CCM yatahadharishwa kuhusu Balozi Mwapachu.

LIVERPOOL YAITUPA NJE MAN UNITED ULAYA

LIVERPOOL imekwenda Robo Fainali ya michuano ya UEFA Europa League baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Manchester United usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford.Manchester United walitangulia kwao bao la kwaju wa penalti la Anthony Martial dakika ya 32, kabla ya Philippe Coutinho kuisawazishia Liverpool dakika ya 45.

Liverpool inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya awali kushinda 1-0 wiki iliyopita Uwanja wa Anfield.  


Tottenham Hotspur nayo imeaga michuano hiyo baada ya kufungwa 2-1 na Borussia Dortmund Uwanja wa White Hart Lane, London. Mabao yote ya Dortmund yamefungwa na Mwanasoka Bora wa Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 24 na 70, wakati la Spurs limefungwa na Heung-Min Son dakika ya 73.


Dortmund inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-1, baada ya wiki iliyopita kushinda 3-0 Ujerumani. 


Sevilla imeifunga 3-0 FC Basel, mabao ya Adil Rami na Kevin Gameiro mawili Uwanja wa Ramon-Sanchez Pizjuan, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya awali kutoa sare ya 0-0 ugenini.


Shakhtar Donetsk imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya RSC Anderlecht, bao pekee la Eduardo Alves da Silva dakika za majeruhi Uwanja wa Constant Vanden Stockstadion, hivyo inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya awali kushinda 3-0 nyumbani.

Sporting Braga imeifunga 4-1 Fenerbahce, mabao ya Ahmed Hassan, Josue Filipe Soares Pesqueira,  Nikola Stojiljkovic na Rafael Alexandre Fernandes Ferreira Silva, huku la wageni likifungwa na Alper Potuk Uwanja wa Estadio Municipal de Braga.

Valencia CF imeshinda 2-1 dhidi ya Athletic Club, mabao yake yakifungwa na Santiago Mina Lorenzo na Aritz Aduriz Zubeldia Uwanja wa Mestalla. Lakini ni Athletic Club, inayosonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2, kufuaia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza.


Sparta Prague imelazimishwa sare ya 0-0 na Dully Sukes, wakati Bayer 04 Leverkusen imelazimishwa sare ya 0-0 na Villarreal BayArena




ATUMBULIWA JIPU KWA KUMDANGANYA WAZIRI MKUU.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jumatano, Machi 2016 akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Chato waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wilayani Chato, mkoani Geita.


Waziri Mkuu ambaye amewasili mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili akitokea mkoani Kagera, alisimamishwa na wakazi wa kijiji cha Kalebezo, kata ya Nyamirembe, wilayani Chato na kukuta mabango yaliyokuwa yakidai maji safi na kuelezea uharibifu wa pampu ya maji.

Katika maelezo yao, wakazi hao walimweleza Waziri Mkuu kwamba mradi wa maji kwenye kata hiyo ulishakamilika lakini pampu yao imechukuliwa na kupelekwa Morogoro jambo lililosababisha wakose maji kwa muda mrefu.

Kwa sababu alikuwa hajafika Chato mjini na hakuwa na taarifa sahihi za mradi huo wa maji, Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi hao kwamba analibeba jambo hilo na atafuatilia hadi aelezwe ni kwa nini pampu hiyo imepelekwa Morogoro.

Akiwa kwenye mkutano wa hadhara, ndipo suala la maji likaibuka tena na Waziri Mkuu kuamua kuchukua hatua hiyo.

“It’s unethical (ni kinyume cha maadili) kumdanganya kiongozi wako. Nimekuuliza mara mbili mbili kama una uhakika kuwa pampu hiyo ipo ukasema una uhakika kuwa ipo. Nimemtuma diwani na vijana wangu wakacheki wakasema hakuna pampu,” alisema Waziri Mkuu na kumwita Diwani huyo jukwaani ili atoe majibu.

“Pale kulikuwa na pampu mbili; moja ni ya kuvuta maji kutoka kwenye kina kirefu na kuyapeleka kwenye pump house na nyingine ni ya kuvuta maji kutoka kwenye pump house na kuyapeleka kwenye tenki kubwa la kuhifadhia maji. Ile ya kutoa maji kwenye kina kirefu ndiyo haipo, wataalamu wanajua wameipeleka wapi,” alisema Bw. Charles Manoni ambaye ni diwani wa kata ya Nyamirembe ambayo kijiji cha Kalebezo kimo.

Waziri Mkuu alisema ahadi ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.
“Lazima watumishi wa umma wabadilike na kuanza kuwatumikia wananchi kwa dhati. Hatuwezi kuwa na watumishi waongo ambao wanamdanganya hata Waziri Mkuu.”

“Kuanzia sasa, Engineer atakaa pembeni, polisi na TAKUKURU wamchunguze. Asitoke Chato hadi uchunguzi ukamilike. Nataka kujua nani alichukua hiyo pampu na kwa kibali gani. Tukijiridhisha atarudi lakini kwa sasa hivi akae kando,” alisema.

Mapema jana mchana, akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Geita na wilaya ya Chato mara baada ya kupokea taarifa zao kwenye ukumbi wa Halmashauri, Waziri Mkuu alimpa fursa Mhandisi huyo aeleze nini kimetokea kuhusu pampu inayodaiwa kupelekwa Morogoro lakini akakanusha na kudai kuwa ipo palepale kijijini.

“Una uhakika na hayo unayoyasema? Hiyo pampu ipo kweli kijijini? Nikienda nitaiona?” alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa mara mbili na mhandisi huyo kwamba ana uhakika asilimia 100 kwamba pampu ipo na wala haijaenda Morogoro.

Alipotaka kujua ni kwa wananchi wa kijiji kile hawana maji kutokana na ubovu wa pampu hiyo, alijibiwa kwamba mradi ule ulikuwa chini ya mamlaka ya maji ya mji wa Bukoba (MBUWASA) ambako wilaya hiyo ilikuwepo zamani kabla ya kuhamishiwa kwenye mkoa mpya wa Geita mwaka 2012.

Mhandishi huyo alisema amekuwa akifuatilia fedha za matengenezo kutoka kwa Mkurugenzi wa MBUWASA bila mafanikio, ndipo Waziri Mkuu akamuagiza aende nje ya ukumbi huo akapige simu na kumletea majibu ni lini fedha hizo zitapatikana ili wananchi wa kijiji kile waendelee kupata maji.

MMALIM SEIF AIONDOA FAMILIA YAKE ZANZIBAR NA KUIPELEKA MUSCAT OMAN.

Pichani ni mkewe Seif Shariff Hamad, Bi Awena Sinani Masoud akiwa chumba cha VIP uwanja wa ndege na tiketi yake ya Oman Air, muda mfupi kabla ya kuondoka.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad ameondosha familia yake katika Kisiwa cha Unguja na kuipeleka Muscat-Oman.

Familia hiyo ya Maalim Seif Shariff Hamad wameondoka jana jioni kwa kutumia ndege ya Shirika la ndege la Oman (Omar Air). Familia hiyo ya Maalim Seif imeondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport saa 5:50 jioni hii.

Haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa za Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad kuiondoa familia yake Zanzibar. Kwa sasa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais yupo katika mapumziko katika Hoteli ya Kitalii ya Dar es Salaam Serena.

AJALI YA BASI YAUA 2 MBEYA.

Watu 2 wapoteza maisha na wengine 12 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Ndenjela kugonga gari dogo aina Hiace mkoani Mbeya. 

STARTIMES KUONYESHA LIGI KUU CHINA LIVE

 Mchezaji wa kimataifa, raia wa Senegal, Demba Ba ni mchezaji nyota aliyewahi kukipiga katika vilabu vya Newcastle, Chelsea na Besiktas kabla ya kuhamia timu ya sasa ya Shangai Shenhua iliyomo katika ligi kuu ya China.

 Mchezaji raia wa Zambia, Jacob Mulenga (pichani) naye anacheza soka la kulipwa katika ligi kuu ya china katika kilabu cha Shijiazhuang Ever Bright.
 Asamoah Gyian, raia wa Ghana pia ni nyota mwingine wa kimataifa kutoka Afrika, yeye kwa sasa anachezea kilabu cha Shangai SIPG ambayo alijiunga nayo mwaka 2015. Gyian ashawahi kukipiga katika kilabu cha Sunderland katika ligi kuu ya Uingereza.
Gervinho baada ya kuchezea timu za Arsenal ya ligi kuu ya Uingereza na AS Roma ya Italia alitimkia ligi kuu nchini China ambako sasa anachezea ligi kilabu cha Hebei China Fortune. (PICHA ZOTE KWA HISANI YA MTANDAO)


Kampuni ya StarTimes Tanzania imewaletea watanzania uhondo wa miongoni mwa ligi ambazo zinajizolea umaarufu kwa kasi hivi sasa duniani, ligi kuu ya China, kwenye chaneli zake za michezo na kuwafanya kufurahia kuona wachezaji nyota kutoka nchi mbalimbali.


Akizungumza juu ya habari hiyo njema kwa wapenzi wa soka nchini, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Lanfang Liao, amesema kuwa ligi hiyo imejizolea umaarufu mkubwa kutokana na wachezaji nyota waliowahi kucheza kwenye vilabu mbalimbali barani Ulaya kukimbilia huko.


“Tunayo furaha kubwa kuwafahamisha wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa tumepata haki miliki ya kuonyesha ligi kuu ya China kwa muda wa miaka mitatu mfululizo na kuonyesha jumla ya michezo takribani 240 moja kwa moja kutoka kwa timu 16 zinazoshiriki. Na tofauti na ligi zingine duniani, ligi hii yenyewe huwa inaanza kwenye miezi ya Machi (msimu wa vuli) na kumalizika Disemba (mapema msimu wa baridi).” Alisema Bw. Liao


Ligi kuu ya China inachukuliwa kuwa ni ya pili, baada ya ligi kuu ya Uingereza ikiitangulia ya Italia, Serie A kwa kuvutia wachezaji wa nje. Ligi hii inalenga kukuza ushindani wenye hali ya juu na pia kukuza ubora wa makocha na wachezaji wa kigeni ambao hatimaye wataweza kujiimarisha katika mfumo wa Uingereza na kuweza kusajili na kuuza wachezaji.


Bw. Liao aliongezea kuwa, “Tunafahamu kuwa watanzania wanapenda sana soka na kama waafrika kwa ujumla wanafurahia sana kuona wenzao wakiliwakilisha bara hili kimataifa. Ligi kuu ya China imejaa waafrika lukuki ambao wanatoka nchi jirani na zinginezo Afrika kama vile James Chamanga na Jacob Mulenga (Zambia), Assani Lukimya (DRC Kongo), Asamoah Gyan (Ghana), Gervinho (Ivory Coast), Demba Ba (Senegal) na nyota wengine kutoka nchi zingine waliowahi kucheza vilabu vikubwa kama vile Ramires, Jackson Martinez, Ezequiel Lavezzi, Paulinho na wengineo.”


“Natumaini kuwa kuja kwa ligi hii kutaongezea burudani ya kutoksha miongoni mwa wateja kwani tulivyokwishawaeleza wateja wetu kuwa siku zote tunapambana kuwapatia mambo mazuri zaidi. Tunafahamu wateja wanahitaji zaidi na zaidi na hata tukilinganisha na jinsi tulivyoanza na tulipofikia ni dhahiri kuwa tumefanya juhudi za kutosha katika kuboresha maudhui ya vipi vyetu. Mpaka sasa ligi ya Bundesliga, Serie A, Ligue 1 zote zinaonekana moja kwa moja.” Alihitimisha Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini


Naye kwa upande wake Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. David Kisaka aliongezea kuwa ujio wa ligi kuu ya China kwenye dikoda za StarTimes umekuja wakati sahihi kwani hivi sasa kuna punguzo kubwa la bei pamoja na ofa ya kuangalia vifurushi vya kawaida na michezo buro ikiwa ni shamrashamra za kuikaribisha sikukuu ya Pasaka.


“Katika kipindi hiki cha Pasaka tumeshusha bei za dikoda zetu za antenna kutoka 34,000/- mpaka 22,000/- tu na kwa upande wa dishi kutoka shilingi 88,000/- mpaka 86,000/- tu. Mteja akinunua bidhaa hizo atafurahia kifurushi cha bure cha chaneli za kawaida pamoja na cha Sport Plus ambacho ataweza kujionea mechi mbalimbali moja kwa moja pamoja na ligi hii ya China ambayo tumewafahamisha.” Alimalizia Bw. Kisaka





Thursday, March 17, 2016

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MWANZA.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea mkoani  Kagera kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akisaini katika kitabu mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Mwanza,mara baada ya kuwasili jijini hapo  jana akitokea Kagera kwa ziara ya kikazi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,ACP Japhet Lusingu(kushoto), akitoa taarifa ya hali ya usalama katika mkoa wa Mwanza kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati) mara baada ya Naibu Waziri kuwasili jijini Mwanza jana akitokea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.Kulia ni Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai mkoa wa Mwanza,SSP Augustine Senga.Add caption

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea Kagera kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MAGAZETI YA LEO> MWAPACHU ARUDI CCM, MAGUFULI AICHOKA IPTL, WARIOBA AMWAGA BUSARA MAHAKAMA YA MAFISADI

Mwapachu arudia kadi yake CCM. Magufuli aichoka IPTL. Warioba amwaga busara mahakama ya mafisadi. DC awasuluhisha Takukuru, polisi.

BARABARA ZA MKOA WA PWANI ZAHARIBIKA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA MAENEO MBALI MBALI

Makamu Mwenyekiti wa  kikao cha bodi ya barabara Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze akifafanua jambo katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akichangia hoja katika kikao hicho cha bodi ya barabara.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kushoto  Zainabu Vulu akiwa na wajumbe wengine waliohudhuria katika kikao hicho, wa kati kati ni Mwenyekiti wa  halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile.(picha zote na Victor Masangu)
Meneja wa wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Tumaini Salakikye akitolea ufafanuai na kujibu maswali yalioulizwa na wajumbe wa kikao hicho juu ya miundombinu ya barabara.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kibaha Leornad Mlowe akitolea ufafanuzi kuhusiana na kero ya ubovu wa barabara katika Wilaya ya Kibaha.
NA VICTOR MASANGU, PWANI  

IMEELEWA kwamba kutokana  na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini zimeweza kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara  na madaraja katika baadhi ya maeneo ya mkoani Pwani hali ambayo imekuwa ni kero kubwa  kwa wananchi kutokana  na magari kukwama hivyo  kutokupitika kwa urahisi.

Hayo yamesemwa  na  Mhandisi mkuu wa kitengo  cha mipango kutoka Wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Zuhura Amani wakati akiwakilisha taarifa ya utekelezaji  wa kazi za matengenezo na miradi ya maendeleo kwa wajumbe  wa kikao cha bodi ya barabara cha Mkoa, ambapo amesema kuwa kuharibika kwa miundombinu hiyo  kunarudisha nyuma jitihada za serikai katika kuleta huduma kwa jamii.

Zuhura alisema    kuwa jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 20.9 zilipangwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014 hadi 2015 lakini kutokana na kuwepo kwa ufinyu wa bajeti zoezi hilo halikuweza kufanikiwa kwa wakati uliopangwa.

Kwa upande wao wajumbe waliohudhuria  katika kikao hicho  akiwemo Mwenyekiti wa CCM  katika Wilaya ya Kibaha Mji,Maulid Bundala  pamoja na Katibu msaidizi wa Mkoa wa Pwani  Shangwe Twamala walisema hai hiyo ya ubovu wa barabara inachangia kwa kiasi kikubwa kukwama kwa magari hivyo kupelekea usumnufu mkubwa hasa katika kipindi cha mvua.

 Nao baadhi wa wabunge wa Mkoa wa Pwani akiwemo Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye ndio alikuwa makamu Mwenyekiti katika kikao hicho alisema kwamba baadhi ya maeneo ya barabara kwa sasa zipo katika hali mbaya ktokana na nyingine kupita kwake ni vigumu kutokana na kuwa na mashimo mengi.

“Kwa hii kwa kweli Meneja na timu yako inabidi kuliangalia kwa macho matatu kwani kuna baadhi ya barabara nyingine katika Mkoa wetu wa Pwani zipo katika hai mbaya sana maana wakati mwingine nashindwa kuelewa tatizo ni nini kwa suala hili naomba mfanya jitihada za kufanya ukarabati ili barabara zetu ziweze kupitaka kwa urais,”alisema Ridhione.

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa alisema kwamba katika jimbo lake kuna barabara ni muhimu sana ya kutoka Nyamwage kulelekea Utete ambapo ndipo makao makuu wa Wilaya hiyo inahitajika ifanyiwe matengenezo ili iweze kupitika kwa urahisi.

“Asilimia 19 la pato la Taifa inategemea katika Wilaya ya Rufiji kutokana na misitu iiyopo hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kabisa kuhakikisha barabara ambazo ni kiunganishi kikubwa zifanyiwe ukarabati na zingine ziwekwe katika kiwango cha lami ili kuweza kuleta chachu ya maenedlea kwa wananchi wa rufiji na Taifa zima kwa ujumla,” alisema Mchengerwa.

 Akijibu malalamiko hayo Meneja wa wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Tumaini Salakikye amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kuongeza kwamba changamoto kubwa inayowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao  ni kutokana na bajeti kuwa ndogo.

Barabara zenye kiwango cha changarawe na  udongo katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani kwa sasa  zimeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hivyo kunahitajika nguvu ya makusudi kutoka serikalini ili ziweze kufanyiwa matengenezo ya haraka.

Wednesday, March 16, 2016

CHAMA CHA MADAKTARI WA AFYA YA KINYWA NA MENO WAKITOA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA KWA WATOTO KITUO CHA ULEMAVU BUHANGIJA

 Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle akizungumza na watoto wanao lelewa katika kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi Buhangija mapema leo asubuhi alipokuwa akiwapa Elimu ya upigaji mswaki na utunzaji wa kinywa  kwa ujumla na utunzaji wa miswaki yao mara wamalizapo kupiga mswaki na kuwaomba japo kupiga marambili kwa siku (POCHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle, akiwatolea mfano kwa Mmoja wa watoto hao
 Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Germana Vincent akigawa flana kwa mtoto mwenye ulemavu wa macho wanao lelewa katika kituo cha Buhangija
 Watoto wenye ulemavu wa ngozi wanao lelewa katika kituo cha Buhangija Mkoani Shinyanga wakiimba nyimbo ya kuwaombea Dua Madaktari hao wakiwa wameinua mikono yao juu

 Baadhi ya Timu ya wasaidizi wa Kituo hicho cha watoto wenye ulemavu wa ngozi akiwemo Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle, (wa pili kulia)
 Kiongozi wa Msafara ambaye pia ni Daktari wa Afya na Kinywa na meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk.  Arnold  Mtenga (katikati) akiteta jambo na madaktari wenzake, kulia ni   Conrad Mselle na kushoto ni Germana Vincent, wote kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili
 Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno, Sr, Benjamini Buya (kulia) wa Hospitali ya Huruma DDH yaWilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro akitoa elimu ya Afya ya Kinywa na Meno kwa Walezi na Wasimamizi wa Kituo hicho
  Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle akimweka ganzi kwa lengo la kumg'oa meno mawili ya mbele
 Profesa Lembariti akimwelekeza mwanafunzi wa kituo hicho cha Buhangija kwa matumizi ya mswaki na kutunza Afya ya Kinywa na Meno huku wanafunzi wengine wakiangalia kwa makini
  Daktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno  Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dk. Nuru Mpuya (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja kwenye chumba cha Ofisi ya Hospitali hiyo na madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kulia ni Mmiliki wa ujijirahaa blog, Kamisi Mussa

  Profesa Lembariti akizungumza na Mtoto Suzy Aseng (8), wa Shule ya Rittle Treasures ya Bungayambelele Darasa la 4, alipokuja katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi Buhangija mara aliposikia kuwa kunamadaktari wa Afya ya Kinywa na Mane watakua  wakitoa huduma ya Afya ya Kinywa na Meno na ndipo alipompa Elimu ya kuhusiana na upigaji mswaki na kumuelekeza mara akiona mswaki unaanza kupinda amwambie mlezi ambadilishie mswaki
 Daktari Wa Fya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili Dr.  Germana Vincent (kushoto) akizungumza jambo na Madaktari wenzake wakati walipotembelea Kituo cha Watoto wenye ulemavy wa ngozi wa Kituo cha Buhangija Mkoani Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa Wiki ya Afya na Kinywa na Meno ambapo kilele cha Maadhimisho hayo yatafanyika Kitaifa Mkoani Morogoro Machi 20, 2016,  kuanzia kulia ni Dr, Gustav Rwekaza wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Daktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno  Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dk. Nuru Mpuya na Dr, Gerald George wa Hospitali ya Jiji la Tanga
Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Manispaa ya Kinondoni Dr. Iddi Khery  akimuhudumia Mmoja wa Mwanafunzi wa kituo cha Buhangija