ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 19, 2016

UKAWA HALI TETE MGOMBEA WA CUF SUMVE AHAMIA CCM.

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Sumve

 ALIYEKUWA  Mgombea Ubunge. wa  Chama Cha Wananchi (CUF)Jimbo la Sumve wilaya Kwimba mkoa wa  Mwanza Richard Ntunduru amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Ntunduru, amehama  rasmi chama hicho Desemba 17 mwaka huu na kupokelewa na viongozi na Wanachama wa Tawi la Mwangika na kukabidhi Kadi na Sare zake zote alizotumia Wakati wa Kampeni mbele ya Halmashauri Kuu ya Tawi na baadaye kwenye Mkutano Mkuu wa Tawi.

  Amewaeleza  viongozi na Wana CCM kuwa, yeye ni Sawa na Mwanampotevu aliyetolewa Mfano kwenye Biblia na kwamba  amerejea Nyumbani kuijenga CCM ambacho ni chama imara kisicho teteleka.

  Akizungumza na Gsengo Blog mara  Baada ya kupokelewa aliahidi kuhakikisha ofisi ya CCM Tawi la Mwangika inakuwa imara kisiasa kwa kiwango kinachopendeza tofauti na ilivyo sasa.

"Nitatoa Ushirikiano kama  ule niliokuwa nikitoa awali kwa Wananchi wote utaongezeka zaidi, lengo ni kuisaidia Serikali ya awamu ya tano, kutekeleza Ilani ya CCM.

  Aidha aliwaomba Wana CCM, kuendelea kujitolea nguvu kazi zao kwenye suala la maendeleo pindi viongozi wao wanapowahitaji kufanya hivyo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.