ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 31, 2016

TRUMP AMSHUKURU PUTIN KWA KUTOWAFUKUZA WANADIPLOMASIA WA MAREKANI.

Donald Trump, Rais mteule wa Marekani jana Ijumaa kupitia ujumbe wa Twitter alimshukuru Rais Vladimir Putin wa Russia kwa kutolipiza kisasi kitendo cha kufukuzwa wanadiplomasia wa nchini hiyo huko Marekani ambacho kilichukuliwa na serikali ya Washington siku ya Alkhamisi, na kusema kuwa daima amekuwa akimtambua Putin kuwa ni kiongozi anayetumia busara.
Huku akitoa radiamali yake kufuatia hatua ya serikali ya Washington ya kuwafukuza wanadiplomasia 35 wa Russia kwa madai ya nchi yao kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekani, Rais Putin amesema kuwa amesikitishwa mno na hatua ya Rais Barack Obama wa nchi hiyo kumaliza kipindi chake cha miaka minane ya uongozi kwa njia hiyo, lakini akaongeza kuwa hatalipiza kisasi kwa kuwafukuza wanadiplomasia wa Marekani wanaohudumu Russia. Akitoa radiamali yake kuhusiana na hatua hiyo ya Putin, Trump amesema kuwa hatua hiyo ya Putin ni nzuri na ya kuvutia sana.
Trump
Katika hali ambayo hatua hiyo ya Putin kutolipiza kitendo hicho cha serikali ya Washingtion haikutarajiwa na wengi katika ngazi za kiaisa za Marekani, lakini hatua ya Trump ya kusifu hatua hiyo imewashangaza hata zaidi na kuwafanya wamtuhumu kuwa anahatarisha maslahi ya kitaifa ya Marekani. 

Ni wazi kuwa huo unaweza kuwa ni mwanzo wa changamoto mpya katika kipindi cha uongozi wa Trump na chama cha Warepublican ambao walimpa madaraka ya kuongoza nchi hiyo. Katika hatua ya hivi karibuni kabisa ya uadui wa Marekani dhidi ya Russia, serikali ya Rais Barack Obama imechukau hatua ya kuwafukuza Marekani wanadiploamasia 35 na kuwawekea vikwazo maafisa sita pamoja na mashirika matano ya Russia kama jibu kwa madai ya nchi hiyo kuhusika na shambulio la kimtandao dhidi ya Marekani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.