ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 8, 2016

MTOTO AFANYIWA UKATILI.

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZINAZOFUATA KWANI ZINATISHA NA KUSIKITISHA ILA ZIMEWEKWA HAPA KWAAJILI YA KUONESHA UKATILI ULIOFANYIKA. @gsengo
  ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza

MTU mmoja aliefahamika kwa jina la Rhoda Juma (30) Mkazi wa Kijiji cha Kilabela Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumfanyia Ukatili Mtoto mdogo wa kike wa mwaka mmoja.

Tukio hilo limetokea Disemba 6,mwaka huu saa nane mchana kijijini humo ambapo mama huyo alimfungia ndani ya Nyumba mtoto huyo kwa muda wa miezi minne na kumshambulia sehemu zake za mwili.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Naibu Kamishina wa  Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema kuwa mwanamke huyo alikuwa akiishi na mtoto huyo Nyumbani kwake baada ya kuletewa na rafiki yake ajulikanae kwa jina moja la Rahel (Recho) ambaye inadaiwa kuwa ndiye mama mzazi wa mtoto huyo.

Amesema inadaiwa kuwa  mama mzazi wa mtoto huyo alimuacha mwanaye Julai mwaka huu na kwenda  kusikojulikana katika shughuli zake za huduma ya baa

“Kwa kipindi chote cha miezi minne mtoto alikuwa akifungiwa ndani na kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake na Rhoda Juma ambaye ni mama alieachiwa mtoto hali iliyopelekea mtoto kuwa na makovu na kudhoofika mkiafya”amesema Msangi.

Aidha Mtuhumiwa amekatwa na atafikishwa  mahakamani ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake na kwamba mtoto amelazwa hospitali ya Wilaya ya Sengerema kwa ajili ya matibabu zaidi.

Hata hivyo Kamanda Msangi amewataka wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuacha vitendo vya ukatili  kwa watoto au watu wazima kwani ni kosa la jinai na kwamba kwa yeyote atakaye bainika atafikishwa kwenye vyombo vya Sheria.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.