ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 12, 2016

MBIO ZA DARAJA LA MAGUFULI MWANZA.

 Kasi ya ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza inaonekana kuwa na matokeo mazuri zaidi licha ya changamoto ya mvua zinazo endelea kunyesha kila kukicha ambazo wengi walidhani zingesimamisha zoezi la ujenzi huo.

Usimikaji wa nguzo mihimili kwa daraja hilo ndiyo umekula muda mrefu tofauti na kazi iliyosalia ya sasa kusimika vyuma vya uundaji daraja.
Hii ndiyo taswira inavyotafutwa.

Ujenzi huo unakwenda sanjari na upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi. 

Mnamo taambayo ujenzi wake  inayo ukabili urehe 11 Agosti Rais Magufuli aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo.

Hili litakuwa daraja la pili kujengwa mkoani Mwanza ikiwa ni mara baada ya Serikali kukamilisha Ujenzi wa Darala la juu la Watembea kwa Miguu katika Eneo la Mabatini wilayani Nyamagana na kupunguza wingi wa ajali pamoja na msongamano wa magari katika eneo hilo, Sasa juhudi zimehamia katika eneo la Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambapo pia linajengwa Daraja la juu la Watembea kwa Miguu ili kukabiliana na foleni katika eneo hilo ambalo limejengwa pia Kitega Uchumi cha Kisasa cha Rock City Mall ambayo ni Mall (Soko) Kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.