ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 11, 2016

HABARI NJEMA KWA WAJASIRIAMALI, WAANDAAJI MKULIMA MARKET WATOA PUNGUZO LA BEI

Mwandaaji wa chapa ya Mkulima Market, Dkt. Vicensia Shule akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza tukio hilo. Kushoto kwake ni  Mratibu wa Vikundi vya Kilimo na Ujasiriamali katika Mkulima market, Steven Peter Mfuko.

Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye Soko la Wazi- Mkulima Market, litakalofanyika tarehe 22, 23 na 24 Desemba 2016 (Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi) katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkabala na UDASA Club huku waandaaji hao wakitoa nafasi 30 kwa wajasiriamai wadogo kushiriki kwenye tukio hilo kwa bei ya punguzo.

Kwa mujibu wa waandaaji wa chapa ya Mkulima Market, Dkt. Vicensia Shule ameeleza amebainisha kuwa,  Habari njema hiyo ni kwa Wajasiriamali wote hapa nchini wameombwa kujitokeza kuchangamkia hofa hiyo.

“Nafasi 30 za Wajasiriamali wadogo wa kilimo, uvuvi, ufugaji na uwindaji kushiriki kwenye Soko la Wazi la Mkulima Market kwa bei ya punguzo. Sasa watalipa 90,000/- tu kwa siku zote tatu kwa banda dogo (mita 2 kwa 6) badala ya 125,000/-

Lipia mapema kupata nafasi hiyo. Wasiliana nasi: Mtayarishaji (simu/sms/whatsapp) kupitia namba 0767 254 887 au Mratibu Msaidizi (Ushiriki) Peter Mfuko 0718 054 169 (simu/sms/whatsapp) au tuandikie: mkulimamarket@gmail.com

Pia tunaendelea kuwashukuru wadhamini wetu kwa kuendelea kujitokeza na  kwa kuwezesha wajasiriamali wadogo kushiriki kwa wingi kwenye onesho hili la Mkulimamarket.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.