ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 11, 2016

CHINA KUJENGA UWANJA WA KISASA WA MPIRA WA MIGUU KWA AJILI YA VIJANA WADOGO KATIKA KIJIJI CHA MSOGA BAGAMOYO


NA VICTOR MASANGU, MSOGA
KATIKA kukuza sekta ya michezo hapa nchini hususan soka la vijana wadogo wa shule  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete  kwa kushirikiana na serikali ya chini watarajia kujenga kiwanja cha michezo cha kisasa katika Kijiji Cha msoga kilichopo halmashauri ya mji mdogo Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Akizungumza katika halfa maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kwenda kutembelea eneo ambalo litajengwa uwanja huo Kikwete amesema kwamba uwanja huo wa wa mpira wa miguu utajengwa  kwa ufadhili wa serikali ya watu wa chini na kuongeza utakuwa ni mkombozi mkubwa katika kukuza na kuinua vipaji kwa vijana wadogo.

Kikwete alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania katika siku za usoni inakuwa ni wachezaji wengi wenye vipaji ambao wataweza kuunda timu nzuri ya Taifa ambayo itaweza kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali ya Kimataifa.

“uwanja huu wa mpira wa miguu pindi utakapokamilika utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa vijana wadogo hususan wale wa shule, hivyo nimeshazungumza na rafiki zetu wa serikali ya china na wamekubali kutujengea kwa hivyo ni jambo la msingi sana katika kuendeleza sekta ya michezo kwa watoto wetu hawa mbao wataweza kuleta mafanikio makubwa katika siku zijazoa,”allisema Kikwete.

Katika hatua nyingine Kikweke  ametoa pongeza kwa serikali ya china kwa kuona umuhimu wa kuweza kusaidia kujenga kiwanja hicho, na kuongeza kuwa pindi kitakapokamilika kitakuwa ni michezo mingine ambayo itakuwa ikifanyika mbali na mchezo huo wa soka lengo ikiwa ni kuwapa fursa vijana kuweza kuonyesha vipaji walivyonavyo.

Naye Mwakilishi wa balozi wa china nchini Tanzania Yang Tong ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kukuza sekta ya mchezo hususan kwa  vijana wadogo ikiwa samba na kujenga viwanja ili watoto wasiweze kucheza katika viwanja vya vumbi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhione Kikwete alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anakuza michezo wa vijana wadogo katika jimbo lake hivyo kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo kutaweza kuwasaidia vijana  kukuza vipaji vyoa.

Nao baadhi ya wadau wa mcheo wa soka katika kiji hicho cha msogo akiwemo i Michael James pamoja na Mohamed Halfan wamempongeza Rais mstaafu Jkaya Kikwete kwa ubunifu wa ujenzi huo wa uwanja kwa ajili ya vijana wadogo kwani kutaweza kusaidia kwa kisi kikubwa katima kuleta mabadiliko chanya katika mchezo huo.

KUKAMILIKA kwa ujenzi  huo wa kiwanja  cha kisasa  cha mpira wa miguu katika kijiji cha soga ambacho alizaliwa rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete kutaweza kutoa fursa kwa vijana wadogo kuweza kukuza na kuonyesha vipaji  walivyonavyo katika medani ya mchezo wa mpira wa miguu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.