ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 16, 2016

CHANGAMOTO YA MAJISAFI, LESENI, VIBALI VYA USAFIRISHAJI NA UMEME VYACHELEWESHA DHAMIRA YA SERIKALI.

Na Peter Fabian, MWANZA.

KAMPUNI mbalimbali za Uwekezaji zilizojitokeza Mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchini zimedai kukabiliwa na changamoto za upatikanaji wa majisafi, leseni, vibali vya usafirishaji nje ya nchi na umeme katika maeneo wanayotaka kujenga viwanda hivyo kuchelewesha dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.

Changamoto hiyo imetolewa na juzi na baadhi ya Kampuni zilizojitokeza kuwekeza viwanda mbalimbali katika mikoa ya Kanda ya Ziwa zilizofika katika Ofisi za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) zilizopo jijini Dar es salaam na Kanda ya Ziwa  ili kupata taratibu na ushauri kabla ya kuanza kujenga viwanda kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kituo cha TIC nchini , Clifford Tandari aliwaeleza baadhi ya wawekezaji waliombioni kujenga viwanda katika mikoa ya Mwanza na Simiyu kuwa dhamira ya serikali ya awamu ya tano ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

Tandari alieleza kwamba amezipokea changamoto hizo za Kampuni ambazo bila kutafutiwa ufumbuzi wa haraka zinaweza kuwakimbiza kna kuacha kuwekeza viwanda katika maeneo mbalimbali nchini hivyo kuahidi TIC kushirikiana na Wizara, Taasisi na Mamlaka zingine za serikali kuhakikisha ucheleweshaji huo unamalizika haraka na kampuni zote zinajenga viwanda haraka kama ilivyokusudiwa na serikali .

“TIC tumejipanga kushughulikia changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka zinazofikisha kwetu na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuondoa urasimu na ucheleweshaji unaoweza kuwakwamisha wawekezaji wa viwanda, hoteli na utoaji huduma nyingine za kijamii,”alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba adhima ya serikali ya awamu ya tano ni Tanzania ya Viwanda  vikubwa, vyakati na vidogo kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo tangu Rais Dk John Magufuli aingie madarakani mwezi Novemba mwaka 2015 hadi sasa Desemba 2016 tayari Kamupini 136 zimejitokeza kuwekeza viwanda.

“Kituo cha TIC kimeisha fikiwa na wawekezaji wa kampuni 136 za ndani na mataifa nje yanayotaka kuwekeza kwa kujenga viwanda vikubwa, vyakati na vidogo hapa inchi nasi TIC tumewahakikishia kuwa tutahakikisha vikwazo na changamoto ikiwemo upatikanaji wa maeneo ya uwekezaji havitakuwa kikwazo kwa,”Alisema.

Tandari ametoa wito kwa Kampuni mbalimbali zinazokusudia kuwekeza kufika katika Kituo cha TIC ili kuwezesha kupata ushauri na kuwasaidia kukamilisha taratibu za kisheria za kuwekeza ili wanapopata matatizo waweze kusaidiwa kwa kuwa wanakuwa na mikataba ya kitaifa na kimataifa ya sheria ya uwekezaji.

Naye Meneja wa TIC Kanda ya Ziwa, Fanuel Lukwalo aliwatambulisha wamiliki na wawakilishi wa Kampuni  za Nyanza Bottiling Ltd (Mwanza) inayotaka kupanua kiwanda kuongeza uzalishaji wa vinywaji baridi, Mwanza Hollidring Ltd inayotaka kujenga kiwanda cha saruji eneo la Nyamatembe lililopo wilayani Busega Mkoa wa Simiyu.

Lukwalo aliwatambulisha Kampuni ya Premidis Ltd iliyo mbioni kujenga kiwanda cha vinywaji vya vileo eneo la Nyakati Wilaya ya Nyamagana na Kampuni ya MRS Wang ya nchini China cha kukausha mabondo ya samaki eneo la Pasiansi Wilaya ya Ilemela, Kampuni ya CMG Ltd ya jijini Mwanza inayojenga kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za saruji .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.