ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 19, 2016

CCM MWANZA KURUDIA UCHAGUZI MDOGO.


Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Mwanza.
NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza

KAMATI ya siasa ya halmashuri kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza imewateuwa Fotnatus Mashauri na Kazimili Komanya kuwa wagombea wa udiwani kata za malya Wilaya ya Kwimba na Kahumulo wilaya sengerema.

Kata hizo zinarudia uchaguzi mdogo mara baada ya tume ya uchaguzi nchini kutangaza nafasi hizo kwa vyama vyote vya siasa ili kuteuwa wagombea wa udiwani kwenye maeneo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake katibu muenezi Mkoani hapa Simoni Mangelepa alieleza kuwa chama cha mapinduzi baada ya kupitia vikao vya kata waliweza kumteuwa kazimili Komanya kwa kura 41 kuwa mgombea udiwani wa kata ya MalyaWilaya ya Kwimba.

Fotnatus Mashauri aliteuliwa na kamati kuu ya CCM Mkoa kuwa mgombea wa nafasi hiyo katika kata ya Kahumulo Wilaya ya Sengerema.

Aidha mangelepa alizitaja sababu za kata hizo kurudia uchaguzi kuwa diwani wa kahumulo Joseph Kando(Njiwa Pori) alijiuzulu kutokana na shughuli zake za kibinadamu kumbana hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa wananchi ipasavyo na kwamba diwani wa Malya Charles Manawa alifariki dunia.

“kwa mujibu wa tume ya uchaguzi tarehe 23/12/2016 ndio tunaanza kampeni hadi 22/1/2017 na ndio itakuwa siku ya uchaguzi wa kuwapata madiwani wa kata hizo mbili ”alisema Mangelepa.

Aliwaomba wananchi na wafuasi wa chama cha mapinduzi kujitokeza kwa wingi na kuwaunga mkono ili kupata viongozi walio bora na makini na kwamba chama kipo pamoja nao ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.