ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 13, 2016

NEC YAFYEKA WAJUMBE.

Dar es Salaam. 
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) iliyokutana leo imeadhimia kupunguza wajumbe wa kamati hiyo kutoka 34 hadi 24 pia wajumbe  wa Halmshauri Kuu kutoka 388 hadi 158.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amewaambia wanahabari leo mbali na hao pia kamati kuu imeadhimia kupunguza wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa na wilaya sanjari na idadi ya vikao.

“Kamati Kuu imeazimia kufanya uhakiki wa wanachama wake, tumeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa wanachama wetu na jumuiya zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama wetu kwa wakati huu kwa sababu kila kukicha wanachama wanaongezeka na kuna hisia wapo wengine ni hewa,” alisema Nape

Aliongeza kuwa uhakiki huo utafanyika kwa kutumia kadi kieletroniki na kuachana na kadi za kawaida na mchakato huo utakwenda sambamba na kufuta kadi za cha jumuiya za chama.

Mbali na Nape ambaye ni Waziri wa Habari, Sanaa ,Utamuduni na Michezo, amesema Mwenyekiti wa CCM Dk John Magufuli amemteua Rodrick Mpogolo kushika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, awali ilikuwa ikishirikiriwa na Rajabu Luhavi aliyeteuliwa kuwa balozi.

Kamati hiyo imemteua Kanali Lubinga Ngemela kuwa Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Dk Asha Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Uingereza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.