ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 21, 2016

OPARESHENI DHIDI YA WAUZA, WAVUTA SHISHA YAENDELEA - SIRRO

Kamanda wa jeshi la  polisi kanda maalumu mkoa wa Dar es salaa,Saimon Siro amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kuwabaini wauzaji wa madawa ya kulevya aina hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Simon Sirro amesema  zoezi hilo bado linaendelea ili kuwabaini wauzaji wa shisha.

Amesema  katika Wilaya ya Kinondoni  wamefanikiwa kuwakamata watu watatu na vielelezo, amesema watawapeleka mahakamani baada ya kupeleka vielelezo kwa Mkemia Mkuu wa serikali na taratibu za mahakamani zitaendelea.

‘’Opareshini dhidi ya shisha bado unaendelea na tunawaomba wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili tuweze kuwabaini wauzaji wa dawa za kulevya aina ya shisha’’  amesema Kamanda Sirro

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.