ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 25, 2016

MWANZA YASISIMKA "YASIMAMA SAA KADHAA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE"

Maandamano ya kusisimua yamefanyika hii leo asubuhi ndani ya jiji la Mwanza ikiwa ni sehemu ya moja ya mikoa hapa nchini ambapo Tanzania imeungana na jamii ya kimataifa kuadhimisha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake huku ndoa za utotoni zikibakia kuwa kikwazo kikubwa kwa mafanikio ya mtoto wa kike ndani ya jamii
Wadau wa kikosi cha Usalama barabarani toka jeshi la polisi mkoa wa Mwanza wameshiriki kikamilifu kuhakikisha zoezi la maandamano toka viwanja vya Ghand Hall hadi uwanja wa Polisi Mabatini linafanikiwa kwa nia ya kuwasilisha ujumbe kwa jamii.
Madereva bodaboda msafarani Maandamano ya Maadhimisho yaliyobeba kauli mbiu FUNGUKA Pinga Ukatili wa Kijinsia Elimu salama kwa wote .
Wadau ndani ya maandamano.
Mwanza imesisimka na kusimama kwa dakika kadhaa kushangaa muonekano wa kuvutia wa maandamano hayo ya maadhimisho ya Siku ya Ukatili Duniani ambapo wadau mbalimbali walijitokeza barabarani wakipiga picha msafara huo. 
 Shirika la Kupinga vitendo vya ukatili kwa Wanawake na Watoto na jamii kwa ujumla KIVULINI ndiyo wamesimamia mpango mzima.
Jeshi la polisi limeonekana kushiriki bega kwa bega kufanikisha dhamira iliyo wekwa.
Wakati maadhimisho haya yakifanyika jijini Mwanza tayari Serikali kupitia wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imeahidi kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971bbkwa lengo la kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni.

Marekebisho hayoyamelenga kumuokoa mtoto wa kike mwenye umri chini ya miaka 18, aliyeko shuleni na ambaye aliyenyumbani dhidi ya ndooa hizo zinazotajwa kuhujumu haki zao za msingi ikiwemo kupata elimu.
'Kikazi zaidi' nia kufanikisha ni Blogger GSengo wa Gsengo Blog.
Taswira.
Wazazi, wanafunzi, wafanyabiashara wadogowadogo na wakubwa wameungana kwa hili.
FICHUA UKATILI WA KIJINSIA UFIKIE MALENGO YAKO YA MAISHA.
Wadau wakitinga viwanja vya kusanyiko.
Kuwa Mwanaume anayempenda na kumjali Mwanamke.
Umoja wa Mataifa pia unatambua umuhimu wa wanawake katika kuwa na sauti sawa kwenye vyombo vya habari. Kwa mujibu wa maazimio ya Mkutano wa Nne wa Wanawake wa Beijing wa Umoja huo wa mwaka 1995, wanawake wanapaswa kuwa na ushiriki kamili na wa usawa katika vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na menejimenti, uandaaji wa vipindi, elimu, mafunzo na utafiti. Kwa mujibu wa maazimio hayo, kuendelea kuandika au kuonyesha mambo mabaya ya wanawake na picha zinazowadhalilisha katika vyombo vya habari kunapaswa kukomeshwa.  

Utafiti pia unasema wanaume wanaongoza kutoa sauti zao katika vyombo vya habari vya Tanzania, wakiwa ni asilimia 79 ya vyanzo vyote vya habari huku wanawake wakishika asilimia 21 tu. Katika suala la ajira katika vyombo vya habari, utafiti unaonyesha kuwa wanawake ni asilimia 36 ya wafanyakazi katika vyombo vya habari, lakini wanashika asilimia 30 tu ya nafasi za juu za utoaji wa maamuzi. 
"Asilimia 57 ya wanawake waliopo kwenye mahusiano wamewahi kutendewa ukatili wa kimwili ndani ya mahusiano hayo na asilimia 18 waliotendewa ukatili wa kingono ndiyo huenda kutafuta msaada wengine wanaona aibu, idadi ni kubwa lakini kunasababu nyingi zinazowafanya kutojitokeza"

"Ukiichukua Kanda ya Ziwa asilimia 50.4 ya wanawake ambao wamewahi kutendewa ukatili wa kimwili wamefanyiwa ukatili huo wakiwa na umri wa miaka 15, Idadi kubwa ya wasichana wanaomaliza darasa la saba kwa Kanda ya Ziwa huishia kutoendelea na elimu ya sekondari na matokeo yake huishia kwenye ndoa za utoto ni au mahusiano ambayo huanza kufanyiwa vitendo vya ukatili wakiwa na umri wa chini"......... By.  Mkurugenzi wa Mtendaji wa Shirika la KIVULINI Yasin Ally akizungumza na wadau walijitokeza viwanja vya Polisi Mabatini Mwanza.


















Polisi Konstebo Oscar Masuya ofisi ya RPC Kitengo cha Dawati la Jinsia akitoa taarifa ya Jeshi la polisi kuhusu vitendo vya uhalifu mkoa wa Mwanza ambapo jeshi hilo limekuwa likitoa msaada kwa waathirika wa vitendo vya ukatili.
Maswali na majibu.
Wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Mwanza wamejitokeza wakiwa na hamasa kubwa.
Ngoma.




Fungua akili.
Wimbo uliovutia ulitoka kwaya hii....
Meza kuu.
Shairi bora.
Takwimu zinaonyesha kuwa kipindi cha mwaka 2016 kuanzia mwezi January hadi mwezi September yameripotia matukio ya ukatili polisi jumla ya makosa 973 ikilinganishwa na mwaka 2015 kipindi kama hicho ambapo yameripotiwa jumla ya makosa 461 tu hivyo kupelekea kuongezeka jumla ya makosa 512 ya kipindi cha mwaka 2016.

Katika kipindi cha mwaka 2016 yapo makosa ambayo yameripotiwa zaidi ukilinganisha na waka 2015, makosa hayo ni ya kulawiti kubaka, kumpa mimba mwanafunzi, kumtorosha mwanafunzi na wazazi au mzazi kutelekeza familia. 

Kuongezeka kwa takwimu kumekuja baada ya juhudi za kutoa elimu kwa wananchi kuongezeka ambapo jeshi la polisi kwa kishirikiana na asasi ya KIVULINI  limeweza kwenda maeneo mengi mkoani Mwanza na kuhamasisha wananchi katika kudhibiti vitendo vya ukatili nao wananchi wakahamasika kutoa taarifa bila shaka.

Bado kuna changamoto nyingi zinazo kabili vita ya kupinga ukatili kwa mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla:- 

1. Jeshi la polisi kutokuwa na ofisi maalum.
2. Kukosekana kwa vitendea kazi ofisi zikihitaji vifaa vya kiofisi vikiwemo vifaa vya kutunzia kumbukumbu kama Computer, kwani taarifa nyingi zinahifadhiwa kwenye mafaili ambayo nayo mara nyingine hupotea au upatikanaji wake wakati wa kufuatilia kesi unakuwa wa kiusumbufu.
3. Mafunzo kwa askari wanaosimamia dawati la jinsia.
4.Kushindwa kutolewa taarifa za ukatili wa kijinsia kwa wakati hivyo kuwa na shaka shaka za kupata ushahidi sahihi.
5. Watu wengi ambao wamekuwa wakitoa taarifa za ukatili wanaporejea nyumbani huamua kurudi nyuma na kumalizana na wahalifu wao kimyakimya nazo kesi kufutwa kienyeji, hali ambayo hulirudisha nyuma jeshi la polisi katika harakati zake za kupambana na uhalifu.
6.Jamii bado haina elimu juu ya vitendo vya ukatili.
7. Wanasheria kuwa yuma katika kusimamia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.