ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 15, 2016

MIRADI 10 YA MAJI YAZINDULIWA MWANZA.
NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza
PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA
GSENGO BLOG.

WAZIRI  wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amezindua miradi 10 ya maji iliyopo milimani yenye thamani ya Sh milioni 751 ambayo itasaidia kusambaza maji safi kwenye Wilaya ya Nyamagana na Ilemela ili kupunguza uhaba wa maji ambao umekuwa ukiwasumbua wananchi waishio  maeneo ya milimani.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Miradi hiyo, Waziri Lwenge amesema kutokana na wakazi wengi wa Mwanza kuishi milimani Serikali kupitia Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mwauwasa wameamua kuondoa adhaa hiyo kwa Wananchi wake na kwamba mwezi disemba mwaka huu ujenzi wa miundo mbinu ya maji taka ili kusafisha mazingira.

Aidha miradi hiyo imefadhiliwa na banki ya ujerumani ya KFW ambapo mwauwasa  walikopa sh milioni 700 huku serikali ikichangia milioni 51 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ili wananchi waapate  huduma ya maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mwauwasa Mhandisi Antony Sanga amesema miradi hiyo ilijengwa kwa maelekezo ya Bodi ya Maji ya Mwauwasa kutokana na Mwaka wa Fedha ulioyopita na wanaamini watapunguza kwa sehemu tatizo la uhaba wa maji kwa wakazi waishio  milimani 

Amesema mwezi disemba wanatarajia kusaini mkataba wa mradi wa ujenzi wa tenki lenye ujazo wa laki nane kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Bugarika, na maeneno jirani huku miradi mingine ya dharula imezinduliwa  Pasiansi, Ibanda, Isamilo, Mahina, Fumagila na Butimba.

Hata hivyo  amesema ifikapo mwaka 2020  asilimia 95za maji safi  na kupunguza upotevu wa maji kutoka 37 hadi 34 mwaka 2017 huku maji taka kutoka asilimia 23 mwaka 2016 hadi 30 mwaka 2020.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.