ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 17, 2016

MARIE STOPES TANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA KUFUNGA UZAZI KWA WANAUME KWA KUTOA HUDUMA HIYO BURE KWENYE MIKOA MITANO BURE NCHINI.

Marie Stopes Tanzania (MST) inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuhamasisha Wanaume Kufunga Uzazi yaani World Vasectomy Day, ili kusaidia wanaume na familia zao kuhamasika kufanya maamuzi sahihi. 

Kufunga uzazi kwa mwanaume yaani Vasectomy, ni njia rahisi, salama na yenye gharama nafuu, lakini imani potofu, vikwazo vya kimila na desturi vimesababisha matumizi ya njia hii ya uzazi wa mpango kuwa chini sana huku baadhi ya wanaume wakiihusisha na kupungua kwa nguvu na hamu ya kufanya mapenzi, au hata kuifananisha na kuhasiwa. 


Utafiti uliyofanyika hivi karibuni na Marie Stopes inaonyesha kuwa baadhi ya wanaume wa kitanzania hawaafiki kufunga uzazi kwa sababu tu ya kukosa elimu stahiki ama kwa uwoga wa njia hii ya uzazi wa mpango, na pengine labda maudhi yatokanayo (kwani wanaume wengine hufikiri kufunga uzazi ni jambo gumu na hatari) au hata kwa kupingwa na wenza wao. 

Pia ilibainika kwamba kuna baadhi ya wanaume wanaogopa mtazamo hasi kutoka kwa jamii inayowazunguka, ikiwa ni pamoja na kutaniwa, kuchekwa, kuonekana kama wamehasiwa, na hawana thamani au nguvu. Hizi zote ni mila potofu.

Ili kuondoa imani hizi potofu na kuongeza uelewa juu ya faida nyingi za njia hii ya uzazi wa mpango, MST imepanga kutoa elimu na huduma za kufunga uzazi bure kwa wanaume katika mikoa mitano ya Tanzania, kama sehemu ya maadhimisho haya ya kimataifa yenye lengo la kuhamasisha wanaume kusimama imara kwa ajili ya watoto, wake zao, pamoja na maisha yao ya baadaye. Huduma hii ya bure itatolewa na timu za mkoba za MST zinazofanya kazi Zanzibar, Kagera, Mwanza na Makambako, pamoja na hospitali ya Mwenge iliyopo jijini Dar es Salaam.

“Vasectomy siyo tu ni moja ya njia bora na uhakika zaidi za uzazi wa mpango, na haisababishi tatizo lolote linalohusiana na nguvu ama hamu ya tendo la ndoa, au nguvu ya mwili wa mtu. Mbinu mpya ya upasuaji bila kutumia wembe na kushonwa iliyobuniwa Marie Stopes International (MSI) hutumia chini ya dakika 15 na ni ya uhakika kwa zaidi ya asilimia 99. Mara nyingi suala la kupanga uzazi limekuwa likionekana kama ni jukumu la wanawake pekee. 


Hata hivyo, wanaume wengi wanhitaji fursa ya kupanga idadi ya watoto wanaowataka, na wanawake wengi wanahitaji washirikiane na wenza wao katika jukumu la kupanga uzazi wa mpango. Marie Stopes Tanzania inapenda kuwahamasisha wanaume ambao wametumia njia hii salama ya kufunga uzazi kuwa mabalozi na kueneza habari wa njia hii ya uzazi wa mpango yenye uhakika na salama pamoja na jinsi ambavyo wamepata amani moyoni mwao,” anasema Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes Tanzania, Bw. Anil Tambay.

Tunapoadhimisha siku ya Vasectomy duniani, MST inaahidi kuwa katika kipindi cha kuanzia sasa hadi 2020, itaongeza jitihada zake katika maeneo makuu yafuatayo:

• Kuzifikia jamii za pembezoni zaidi na vijijini kwenye mahitaji ya huduma za uzazi wa mpango kwa wanawake na wanaume hasa wale wanaoishi kwa kipato cha chini ya Dola 1.25 (Shilingi 2,730).

• Kufanya kazi na mamlaka za serikali katika ngazi ya taifa, mkoa hadi wilaya ili kuboresha huduma. Zaidi ya watoa huduma 600 wa sekta ya umma wamepatiwa mafunzo katika mwaka 2015 na wanaendelea kutoa huduma. Watoa huduma wengine zaidi wanatarajiwa kupewa mafunzo ikiwa ni sehemu ya mchango wetu katika kujengea uwezo sekta ya umma.

Takwimu za mfumo wa taarifa za afya za wilaya nchini (DHIS 2) kwa miaka mitano iliyopita, zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko la wanaume wanaofanyiwa njia ya kufunga uzazi, kutoka wanaume wawili (2) mwaka 2011 hadi 905 mwaka 2015, na 1079 kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu. Takwimu hizi pia zinaonyesha kuwa mkoa wa Kigoma umekuwa ukifanya vizuri kwa kuwa na mwitikio mkubwa wa wanaume kufunga uzazi, ukifuatiwa na mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Kagera.

Wakati huo huo, takwimu za mfumo wa taarifa za afya za Marie Stopes Tanzania pia zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko la wanaume wanaokubali kufunga uzazi ambapo jumla ya wanaume 598 wamepatiwa huduma hiyo kati ya mwaka 2012 na October 2016, katika Zahanati na huduma za mkoba za Marie Stopes katika maeneo mbalimbali hapa nchini.za kijinsia, afya ya uzazi na uzazi wa mpango katika maeneo ya mijini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.