ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 14, 2016

MAMA SAMIA KUZINDUA KAMPENI YA KUPIMA SARATANI YA MATITI KESHO.

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, anatarajia kuzindua kampeni ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi hapo kesho kwenye uwanja wa furahisha Mkoa wa Mwanza.

Uzinduzi huo wenye lengo la kupunguza vifo vya wanawake vitukanyo na saratani kufuatia kasi ya ugonjwa huo kushamili kwa wanawake huku akina mama 1294 a mwaka 2011/2012 walifikiwa na huduma  kati ya hao 58 walionekana kuwa na saratani 45 walitibiwa na 13 walipatiwa Rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwaajili ya matibabu zaidi.


Akizungumzia ujio huo, Rais wa Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) Dk. Serafina Mkuwa ameeleza kuwa nia ya shirika hilo ni kupima saratani ya matiti wanawake wapatao 3, 000 na mlango wa kizazi 1200 Mkoani hapa.

Zoezi hilo litafanyika kesho na November  16, katika vituo vinne vya Makongoro, Igoma,  karume na kituo cha furahisha ambapo uzinduzi rasmi utafanyika

Alieleza kua miongoni mwa wanawake ambao wamekuwa wakikumbwa na tatizo hilo, ni wale walio na umri wa miaka 30-50 na kwamba pamoja na hayo, wapo pia ambao huupata wakiwa chini ya umri huo huku akiwaasa wanawake kujitokeza kwa wingi kupima Afya zao.

Alifafanunua kwamba huduma zitakazo tolewa in pamoja na utoaji wa elimu juu ya ugonjwa wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi na pia kutoa huduma ya uchunguzi wa awali wa magonjwa hayo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Leonard Subi  alieleza kuwa mkoa una vituo 20 vinavyotoa huduma ya uchunguzi wa saratani na kwamba zoezi hilo ni endelevu na litakuwa likifanyika katika vituo  vyote vya afya vilivyopo mkoani hapa.

"Zoezi hili limekuwa likifanyika mara kwa mara katika mkoa wa Mwanza lakini kwa sasa tunaaza kwa kampeni ambayo itahamasisha wananchi, wananwake kujitokeza kwa wingi ili kujua afya zao na pia kuepuka vifo vya mama ambavyo vimekuwa vikitokea"alisema Subi

Aidha amesema Magonjwa yasiyo ambukiza yamekuwa yakisababisha vifo vya wanawake kwa asilimia 27 na kwamba yamekua ni janga hivyo ni vyema wananchi na wakazi wa mkoa wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kupima na kufahamu dalili za ugonjwa ili kukabiliana nalo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.