ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 15, 2016

MAMA SAMIA ATUA MWANZA KUSHIRIKI KAZI ZA KIJAMII IKIWA NI PAMOJA NA KUILINDA AFYA YA MAMA.

Makamu wa Rais Mama SAMIA SULUHU HASSAN amewasili jana jioni mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku 6 ambapo atazungumza na wananchi na kuzindua miradi ya afya, elimu na kuweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji wilayani Ukerewe.


Akiwa jijini Mwanza leo mama samia atazindua kampeni ya kupambana na Saratani ya titi na mlango wa kizazi na kuzungumza na wakazi wa jiji la Mwanza katika viwanja vya Furahisha kabla ya kuelekea wilayani Sengerema.

Katika kile kinachoonekana ni kubana matumizi ya serikali ya awamu ya tano, makamu wa rais mama SAMIA SULUHU HASSAN ametumia ndege ya abiria kutoka DSM kwenda Mwaza kwa ziara ya kikazi.

Aidha Mama Samia akaeleza tajiriba yake ya kutumia ndege mpya za ATCL Bombardier DASH8-Q 400. BOFYA JIONEE KATIKA VIDEO.


Akiwa Mkoani Mwz Makamu wa rais mama samia anatarajiwa kuzungumza na wananchi katika viwanja vya Furahisha ambapo atazindua kampeni ya kupambana na saratani ya titi na shingo ya kizazi.

Kwa mujibu wa ratiba Makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Mwz anatarajiwa kutembelea Sengerema, Ukerewe, Misugwi na Magu.

PICHA NA HABARI: ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.
Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.