ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 22, 2016

KOCHA BRUCE ARENA NDIYE MRITHI WA KLISHMANN ALIYETIMULIWA MAREKANI.

Kwa mujibu wa mtandao wa Goal, Bruce Arena ndiye anayetajwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Marekani kufuatia kutimuliwa kwa Jurgen Klinsmann.
Arena, ambaye alikuwa kocha wa taifa hilo kwenye World Cup ya mwaka 2002 na 2006, ataachana na waajiri wake wa sasa LA Galaxy na kurithi mikoba ya Jurgen Klinsmann. Taarifa rasmi inatarajiwa kutolewa leo.

Marekani wameamua kuachana na Klinsmann kufuatia matokeo mfululizo yasiyoridhisha katika michezo ya hatua ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia.
Kwa haraka haraka watu waliopitia mikononi mwa Bruce katika zama zao za kumalizia soka ni pamoja na David Beckham, Ashley Cole na sasa Steven Gerrard.

Kufuatia kupoteza michezo miwili mfululizo ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, ikiwemo mchezo wa nyumbani dhidi ya Mexico na ule wa kipigo cha 4-0 kutoka kwa Costa Rica, maafisa wa Soka Marekani wameamua kusitisha mkataba wake ambao ulikuwa ufikie kikomo mwaka 2018 baada ya Michuano ya Kombe la Dunia.

Arena (65), ambaye ameshinda mataji matano ya MLS akiwa na Galaxy na D.C. United, hivi karibuni alisaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuifundisha LA Galaxy. Hata hivyo ni vigumu sana kwa kocha huyo kukataa ofa ya kulinoa taifa hilo na kuendelea kubaki Galaxy.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.