ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 8, 2016

KENOPI YA GHOROFA YAUWA WAWILI.

NA ANNASTAZIA MAGINGAMwanza

WATU wawili jijini Mwanza wamefariki dunia katika ajali ya kuangukiwa na kenopi ya jengo la ghorofa moja wakati wakiendelea na shughuli za ujenzi katika nyumba hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kaimu kamanda wa polisi Mkoani hapa Augastino Senga amesema tukio hilo limetokea juzi saa 11:30 asubuhi katika eneo la mtaa wa Buganda kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.

Imedaiwa kuwa marehemu walikuwa wamepewa kibarua hicho na mmiliki wa jengo hilo Gaston David (56) ghafla ndipo ajali hiyo ilitokea hadi kupelekea wote wawili kupoteza maisha.

Kaimu Kamanda amewataja marehemu kuwa ni Twalib Nassib (18) na Yusuph Masunga (32) wote vibarua wa ujenzi na wakazi wa Buganda kata ya Mkolani na huku chunguzi wa awali ukibainisha chanzo cha ajali hiyo ni ujenzi wa jengo uliokuwa chini ya kiwango.

Aidha jeshi la polisi linamshikilia mmiliki wa jengo hilo kwa mahojiano zaidi na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi.

Hata hivyo kaimu kamanda Senga amewataka wananchi wa jiji la Mwanza kuwa makini wakati huu wenye mvua kuacha kukaa katika maeneo hatarishi ili kuepuka vifo na ajali zinazoweza kuepukika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.