ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 7, 2016

JAMII YASHAURIWA KUACHANA NA IMANI POTOFU

NA ANNASTAZIA MAGINGA, KWIMBA 

JAMII imeshauriwa kuachana na imani potofu za kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu na badala yake wapewe nafasi katika ngazi ya maamuzi na shughuli za maendeleo ili kujenga jamii yenye usawa. 

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Mwabomba wilayani Kwimba mkoani hapa, Afisa Ustawi wa Jamii, Salum Liundu alisema kuwa jamii inapaswa kuondokana na mila potofu.

 Alisema kuwa mara nyingi jamii udhani familia kuwamo mtu mwenye ulemavu ni laana na pengine kumnyima haki naikiwa kufanya hivyo ni kumyanyapa ni jambo linalopaswa kupigwa vikali. “Binadamu wote ni sawa,hii dhana ya kumtenga na kumyanyasa mtu mwenye ulemavu inapaswa kupingwa katika jamii kwa nguvu zote,haki ni kwa kila mmoja wetu”alisema Liundu . 

Mkutano huo uliandaliwa na chama cha wasioona wilaya ya Kwimba (TLB) kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society (FCS) ukiwa na lengo la kujenga jamii moja shirikishi kwenye vyombo vya maamuzi. Malengo mengine ya mikutano hiyo ni kuchambua na kujenga ufahamu na hamasa kwa jamii kuhusu sera na sheria ya watu wenye ulemavu katika kupanga mipango ya maendeleo jumuishi.

 Mratibu wa mradi wa Ushawishi na Utetezi kwa watu wenye ulemavu Kwimba,Isack Manumbu alisema kuwa kupitia mikutano wanatarajia kupata idadi kamili ya watu wenye ulemevu katika wilaya nzima ikiwa na kuwapeleka shule wanaopaswa kuwa shule ili kuwajengea uwezo wa kuondokana na ushawishi. 

Pia alisema kuwa elimu watakayotoa ana imani kutapunguza vitendo vya unyanyapaa na unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wenye ulemavu katika jamii yenye maendeleo ili kujenga taswira nzuri ya uhirikishwaji kwenye ngazi zote. 

 Anastazia Costantine amabye ni mlemavu wa ngozi (Albino) alishukuru kutolewa kwa elimu hiyo baada ya kusikitishwa na kitendo cha kuitwa majina ya kibaguzi na kutengwa kushiriki kwenye shughuli mbalmbali za kimaendeleo kijijini hapo kama kushiriki kwenye vikundi vya akina mama na misibani.

 “Binafsi nalipongeza hili shirika kwani hapo nyuma nimekuwa nikiishi kinyionge kutokana na jamii kunichukulia mimi kama mkosi maana hata wakina mama wenzangu wamekuwa wakininyima kushiriki kwenye vikundi vyao wkiniambia nafasi zimejaa angali watu wakawaida wamekuwa wakipewa nafasi alisema”, Anastazia. 

Kwa upande wake mwezeshaji wa mradi huo Alexender Maningu alisema hata wahanga ambao ni walemavu wenyewe hawajua jinsi ya kudai haki zao hivyo kupitia elimu hii wanaiyoitoa ana imani dhana hiyo inaenda kufutwa na kujenga jamii moja Mwisho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.