ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 16, 2016

DR. KIGWANGALLA NA TIMU YAKE WANASA KIWANDA CHA KUTENGENEZA POMBE FEKI.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla  akiwa ameshika vifuniko vya bidhaa za pombe feki katika moja ya kiwanda bubu cha kutengeneza pombe hizo aina ya Konyagi. katika zoezi hilo eneo la Sinza.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, akiwa ameongzana na timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama wameendesha operesheni kali ya kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam  na kufanikiwa kukama sehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo  hayo.

Katika operesheni hiyo, pia wamefanikiwa kukibaini kiwanda bubu kinachotengeneza kinywaji aina ya konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza Jijini Dar  es Salaam. 

whatsapp-image-2016-11-15-at-16-43-59
Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia ‘spirit’ ambayo inachanganywa na ‘gongo’; spirit, gongo, chupa tupu na zilizojazwa, vizibo, vifungashio vimekamatwa.

Kwa hatua hiyo Jeshi la Polisi inawashikilia watu wawili ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na polisi mpaka sasa kwa tuhuma za kuendesha shughuli hizo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua bidhaa za feki akiwa pamoja na maafisa wengine katika zoezi hilo eneo la Sinza.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla amezifuma bidhaa hizi feki akiwa pamoja na maafisa wengine katika zoezi hilo eneo la Sinza.
Sehemu ya shehena za bidhaa za feki zikiwa pamoja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.