ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 14, 2016

WAZIRI NAPE AKANYAGA NYAMAGANA.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiendesha kidampa, huku msafara wa viongozi walioongozana naye akiwemo Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ukimfuatilia ni jana wakati alipotembelea uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza, ili kujionea zoezi la uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja huo.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameeleza kuridhishwa na uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja huo ambapo amewashukuru wadau wote waliofanikisha ukarabati wake wakiwemo wajasiriamali Jijini Mwanza ambao kodi zao zimesaidia upatikanaji wa zaidi ya shilingi Milioni 190 kutoka Halmashauri ya Jiji hilo ambazo zilizojumuishwa na dola za Kimarekani Laki Tano zilizotolewa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
 
Altaf Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia ukarabati wa uwanja huo ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Wadau wa michezo Jijini Mwanza wamefurahishwa na uwekaji nyasi kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana ambao ulianzishwa mwaka 1945 ambapo wamesema utaongeza chachu ya ongezeko la mechi za mpira wa miguu Jijini Mwanza pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato pia.
Waziri Nape akisaini kitabu cha wageni wilaya ya Nyamagana mbele ya Diwani wa Kata hiyo Bhiku Kotecha. Itakumbukwa kwamba nyasi bandia kwa ajili ya uwanja huu zilikwama bandarini kwa muda mrefu baada ya TFF kutakiwa kulipiwa kodi ya zaidi ya shilingi Milioni 32 hali ambayo ilisababisha utekelezaji wake kusuasua.
Altaf Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia ukarabati wa uwanja huo ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Waziri Nape Nhauye amesema Serikali itaendelea kuboresha viwanja mbalimbali nchini ikiwemo kushirikiana na makampuni mbalimbali ili kukarabati viwanja vilivyopo ili Tanzania iwe sehemu bora hata kwa mataifa mengine kufika kwa ajili ya mazoezi na michezo mbalimbali hususani ya mpira wa miguu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati aliyenyoosha mkono), akizungumza na wadau alipotembelea uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza hii leo ili kujionea zoezi la uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.