ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 12, 2016

ALIYEUA MTU CHUMBANI AKAMATWA NA POLISI.

JESHI la Polisi mkoani Manyara, limemkamata mhusika wa tukio la mauaji ya mtu aliyekutwa chumbani akiwa amekufa huku mwili wake ukiwa sakafuni pembeni ya kitanda katika mtaa wa Negamsi, kata ya Bagara, mkoani humo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 30, mwaka huu, saa nne asubuhi ambapo, Alex Charles (27), mkazi wa mtaa wa Negamsi katika kata ya Bagara, tarafa ya Babati alikutwa chumbani kwake amekufa.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Francis Massawe akizungumza na gazeti hili jana alisema, mtu huyo alikutwa ameuawa na watu wasiojulikana nyumbani kwake kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika paji lake la uso na kuvunjwa taya la upande wa kushoto na kusababisha kuvuja damu nyingi, hatimaye kupoteza maisha.

Alisema mtuhumiwa huyo ambaye jina limehifadhiwa kwa ajili ya upelelezi, anadaiwa alikuwa mtu wa karibu na familia ya marehemu na alikuwa akiishi nayo kwa muda mrefu, na alipohojiwa alikiri kuua na kwamba alifanya hivyo kwa kujitetea kutokana na kutaka kumlawiti.

Kamanda Massawe alieleza kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa Novemba 8, mwaka huu, akiwa na mali alizoiba katika nyumba ya marehemu zikiwamo pasi ya umeme, deki, viatu na suruali ya jeans, sweta na koti moja la marehemu.

Vifaa hivyo vilitambuliwa na mke wa marehemu na muuaji huyo, ambapo mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na mauaji hayo peke yake na kisa ni kwamba alikuwa ametishwa na marehemu kuwa atamuua kwa mkuki na katika kujitetea ndipo akamwahi.

Mtuhumiwa huyo aliendelea kueleza kuwa Alex, alipokuwa naye chumbani kwake siku ya tukio, alitaka kumlawiti na walibishana naye kitambo, ndipo akamsukuma na kumbamiza ukutani na kupiga yowe.

Katika hatua nyingine, Kamanda Masawe alisema, Matayo Yohana (19) dereva bodaboda akiwa njiani alisimamishwa na mtu aliyejifanya abiria na ndipo watu wengine wanne walijitokeza na kuanza kumpiga na kumjeruhi mguu wa kushoto.

Alisema watu hao walipora pikipiki hiyo yenye namba za usajili MC 500 AYH aina ya King Lion, mali ya Joachim John, baada ya kuporwa, msako ulifanyika kwa kushirikiana na wananchi, ndipo watuhumiwa tatu walipatikana wakiwa na pikipiki nyingine mali ya Edmund Peter (40) yenye namba za usajili T814 CCM.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.