ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 16, 2016

WATU 21 WAFARIKI DUNIA + IDADI YA NYUMBA ZILIZOZAMA HAIJULIKANI.

 Mafuriko makubwa katikati mwa taifa la Vietnam yamesababisha vifo vya watu 21 huku makumi ya maelfu ya nyumba yakizama.
Mkoa wa Quang Binh ndio ulioathirika sana huku watu 11 wakifariki ,mimea kuharibiwa na mifugo ikisombwa na maji.
Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha ,lakini vyombo vya habari vinasema kuwa maji yaliotoka katika hifadhi za umeme yalichangia pakubwa mafuriko hayo.

Kimbunga Sarika huenda kikasababisha hali mbaya ya anga iwapo kitapiga Vietnam.

 Siku ya Jumapili kimbunga hicho kilipita katika kisiwa cha Luzon na kuelekea katika bahari ya kusini mwa China.
Maelfu ya raia wa Filipino waliondoka katika maeneo ya chini huku kuharibika kwa mali,kuzama kwa miti ya stima na kuanguka kwa miti kukiripotiwa.
  Beseni linapotumika kama chombo cha usafiri na kujisitiri.

  Makazi yote yamefunikwa na maji nayo mitumbwi imechukuwa nafasi ya magari, baiskeli na pikipiki linapoitwa suala la usafiri na usafirishaji.

 Baadhi ya kaya zimelazimika kuishi kwenye paa na dari za nyumba kufuatia maji kujaa kwenye maeneo yao wakikosa huduma muhimu kama chakula, maji salama, sehemu za kulala na umeme kwaajili ya mwanga na kuendesha shughuli zao za maisha za kila siku.

Miundombinu ya reli na barabara imeharibika vibaya na kuna kuna hali ya hatari kurejea katika hali ya kawaida.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.