ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 23, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: IDD AZIZ AACHIA WIMBO MPYA “TABIA”

Mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Idd Aziz kutoka nchini Kenya ameachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Tabia.’ Ukihusu lugha adhimu ya Kiswahili, wimbo huu umeanikwa katika lugha tamu ya Kiswahili kwa wapenzi wa muziki na wajuzi wa lugha hiyo duniani kote.

Idd anauelezea TABIA, “Nilitaka kutengeneza wimbo ambao hautaishia kuwa mzuri tu lakini pia uwe na ujumbe mkubwa utakaodumu kwa vizazi zijazo.  Nahisi kuwa ujumbe iliyopitishwa kwenye wimbo huu ni jambo ambalo sote twapitia, haswa vijana katika jamii.”

Ukiandikiwa na kuimbwa na  Idd Aziz, TABIA umetayarishwa na Jesse Bukindu huku video yake ikitarajiwa kupepea hewani mwezi wa Desemba mwaka huu. 

Idd anatueleza: ‘’Nilikutana na binti mmoja mrembo sana. Nilimpeleka kwa wazazi wangu, akajulikana na baba na mama. Nikamwonyesha rafiki zangu, lakini ndugu zangu wote walimkataa aka vunja vunja vikombe. Kumbe sikujui tabia yake mbaya kwa vile alikua amenichanganya na urembo wake!


TABIA ni wimbo halisi wa Kikenya wenye vionjo vya Afrika Mashariki. “ Wimbo na ujumbe wa wimbo huu vimeshiba. Naamini mtaupenda. Nitaendelea kuachia nyimbo nzuri za Kiswahili,” anasema Iddi.

Idd Aziz amekua akicheza na bendi maarufu ‘Charanga Habanera’ ndio maana TABIA imeundwa kwa ladha ya Afrika na Latin.


SKILIZE KISWAHILI kwenye Mkito: https://mkito.com/song/ 13853

SIKILIZE KISWAHILI kwenye Soundcloud: https://m.soundclo ud.com/iddaziz/tabia

Tafadhali pokea wimbo na posta yake vilivyoambatanishwa kwenye wimbo huu. Kuwa huru kuusambaza ndani ya mitandao yako.

DOKOZE KWA WAHARIRI:

Idd Aziz ni miongoni mwa wacheza ngoma maarufu Kenya akiwa mkuu wa bendi yake mwenyewe huku pia akiwa mcheza ngoma wa Sauti Sol. Kwa sasa anazunguka na kundi la Sauti Sol barani Afrika kwenye ziara yao, Live and Die in Afrika. Kando na kucheza na Dj maarufu (Mshindi wa tuzo la Grammy), Idd ametumbuiza mara nyingi kwenye ziara za Afrika, Ulaya na Amerika. Amefanya kazi na wasanii nguli akiwemo, Whitney Houston, Haddaway, Salif Keita, Mercy Myra, Fumio (Japani), Henning Siumaro and Trondheim Orchestra,  STL,
Khaligraph JoneS, Kunguru na Neccessary Noize . Anasema anaendelea kujiimarisha pia kama mwanamuziki wa kujitegemea na kuingia studio kurekodi zaidi.

Fuate Idd Aziz kwenye mtandao: Instagram na Twitter: @iddaziz | Facebook: Idd Aziz | Youtube: Idd Aziz | Mkito: Idd Aziz

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.