ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 7, 2016

MZEE NGASSA AANZA VYEMA KIBARUA CHAKE NDANI YA TOTO AFRICANS YAITANDIKA KAGERA 0-2 UWANJA WA KAITABA.

Baada ya kocha wa awali Mzee Kaijage kuamua kumwaga manyanga kuifundisha klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza ikiwa ni kufuatia kuvurunda mfululizo kwenye michezo yake ya awali, hii leo raha imeibuka kwa kocha mpya wa timu hiyo, Khalfan Ngassa ambaye ni baba mzazi wa kiungo mshambuliaji wa Fanja FC ya Oman, Mrisho Ngassa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera.

Mabao ya Toto yalifungwa na Jamal Soud dakika ya 47 na Mohammed Soud dakika ya 80.

Kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Stand United ya Shinyanga imeonyesha imebadilika msimu huu baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya wenyeji wake Mbeya City.

Mbeya City sasa imebaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 16 moja nyuma ya vinara Simba. Mbeya City imepaa hadi nafasi ya nne na pointi 12.

Stand United imeendeleza rekodi yake ya kutofungwa msimu huu kwani imecheza mechi nane na imeshinda nne na kutoka sare nane.  Mbeya City imecheza mechi nane, imeshinda tatu, sare tatu na kufungwa mbili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.