ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 19, 2016

MISS TANZANIA 2016 MWANZA IMEPANGWA KUVUNJA REKODI.

Leo Oktoba 19, 2016 Kamati ya Shindano la Maandalizi ya Miss Tanzania 2016 imesema Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29,10, 2016 katika viunga vya Rock City Jijini Mwanza, litakuwa bora zaidi kutokana na maandalizi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hashim Lundenga (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Rhino Agency inayoandaa Miss Tanzania, amesema baada ya mashindano hayo kufanyika Jijini Dar es salaam miaka yote, kamati hiyo imeamua yafanyike Jijini Mwanza na kwamba yatafanyika kwa miaka mitano mfululizo.

Amesema washiriki wote 30 katika shindano hilo ni bora hivyo yeyote atakayeibuka mshindi ataliwakilisha vyema taifa kwenye mashindano ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika Disemba 18, 2016 Jijini Washingtone DC nchini Marekani.

Viingilio katika shindano hilo ni shilingi 20,000, 50,000 na 100,000 ambapo inategemewa kwamba wasanii Ali Kiba pamoja, Christian Bella pamoja na mwimbaji wa Ragga anayetikisa toka Rock City ambaye pia ni mtangazaji wa Jembe Fm Cooly Chata watadondosha burudani katika shindano hilo huku washiriki wakijipatia fursa mbalimbali ikiwemo mshindi wa kwanza kujishindia gari.

Washiriki wa shindano hilo wamesema wamejiandaa vyema na bado wanaendelea kujinoa zaidi ili kuhakikisha atakayeibuka mshindi anaiwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano ya dunia huku wakielezea furaha yao kubwa kwa mashindano hayo kufanyika Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza.

Kamati ya Miss Tanzania 2016  Pamela Irengo mwenye kipaza sauti na Flora Lauwo.
Flora Lauwo.
Meneja wa vipindi Jembe Fm Timoth Ngalula (kulia) akifafanua jinsi vitengo vya burudani vilivyojipanga ili kuleta utofauti siku ya tukio.

Baadhi ya washiriki wa Miss Tanzania 2016 katika ubora wao
Hapo vipi.
Ni yupi...
Hatariii...
Debe.....
Washiriki wa Miss Tanzania 2016 katika ubora wao

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.