ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 19, 2016

MCHENGERWA AHAHIDI KUWASAIDIA WAKINAMAMA WAJASIRIAMALI RUFIJI KWA AJILI YA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Mbunge wa jimbo Rufiji Mohamed Mchengerwa kulia akimkabidhi mmoja wa viongozi wa kikundi cha wakinamama wajasiriamali  katika kijiji cha Mloka cheki ya kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya kuwasaidia kuwainua kiuchumi na kukuza mtaji wao. PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa  wa kati kati akiwa  katika picha ya pamoja na badhi ya wakinamama baada ya kufanya ziara yake ya kuwatembelea kwa ajili ya kuweza kubaini chanagamoto zao zinazowakabili. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
MBUNGE  wa jimbo la rufiji Mohamed Mchengerwa ameahidi kuvisadia vikundi mbali mbali  vya wakinamama wajasiriamali  kwa lengo la kuweza kuwainua kiuchumi na kuweza kuinua  mitaji waliyonayo ili kuondokana na janga la umasikini na  kuwa tegemezi.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuwatembeea wananchi wa jimboni kwake kwa ajili ya kuweza kubaini changamoto mbali mbai zinazowakabili kwa lengo la kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Alisema kuwa katika jimbo lake la rufiji kuna vikundi mbali mbali vya ujasiriamali hivyo atajitahidi kwa hali na mali kuvisaidia kuviwezesha fedha ambazo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kaatika shughuli zao za kila siku na kuleta mabadiliko chanaya ya kimaendeleo.

“Mimi kama mbunge wa jimbo la rufiji wananchi mmenipa dhamana kubwa ya kuwatumikia hivyo kwa upande wangu nitahakikisha yale yote ambayo nimewea kuwaahidi wakati wa kampeni nitayafanyia kazi kwa vitendo, na ninahitaji wakinamama wote mjiunge katika vikundi ili iweze kuwa rahisi katika kuwasaidia kuliko mtu mmoja mmoja,”alisema Mchengrwa.

Aidha aliongeza kuwa ana imani endapo vikundi hivyo vya wakinamama vikiwezeshwa vitaweza kupiga hatua kubwa ya kuweza kujiajiri wao wenyewe na kuendesha biashara zao ambao zitaweza kuwapataia kipato amabcho kitaweza kusaidaia katika kuendesha familia zao kuliko ya kuwa na tabia ya kuwa tegemezi kwa watu wengine.

Alisema kuwa japo anatambua wananchi wa jimbo lake wanakabiliwa na changamoto mbali mbali lakini kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya tano atashirikiana nayo bega kwa bega kwa lengo la kuweza kuleta maendeleo makubwa  katika  Wilaya ya Rufuji.

Aidha katika hatua nyingine Mchengerwa katika ziara yake hiyo aliweza kukitembelea kikundi cha wakinamama wajasiriamali  katika  kijiji cha mloka na kukikabidhi kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kuweza kukuza mtaji wao pamoja ana  kujiendeleza  zaidi katika kukuza biashara zao wanazozifanya  kila siku.

Pia  mbunge huyo aliwahimiza wakinamama wa wilayani Rufiji kuhakikisha  fedha hizo zilizotolewa kwa ajili ya kikundi zinatumika vizuri bila ya kuwa na ubaguzi wa aina yoyote  na badala yake zitumike kwa manufaa ya wanachama wote ambao wanatarajia kujikwamua kiuchumi na kuweza kuondokana na tatizo la umasikini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.