ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 17, 2016

MAKAMBA AMWAGA MIFUKO 100 YA SEMENTI KATURUKILA.

Kilombero.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mazingira na Muungano), January Makmba ameahidi kukikabidhi mifuko 100 sementi Kijiji cha Katurukila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya baada ya wanakijiji kuonyesha mwamko wa kutunza mazingira.
Akiwa katika kijiji hicho, kilichopo  Tarafa ya Mang'ula Makamba alisema  amefurahishwa na mwamko waliokuwa nao wakazi wa Katurukila wa kutunza mazingira bila kushurutishwa

"Hivi mnaweza kuniambia mnataka zawadi gani? Akajitokeza mwanakijiji mmoja Amir Mwema na kusema Mheshimiwa (Makamba) kituo chetu cha afya hakipo katika hali nzuri tunaomba utusaidie.

Makamba  alikubali ombi  hilo na kuwaahidi mifuko hiyo itakwenda Katurukila  baada ya wiki moja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.