ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 17, 2016

LIVERPOOL KUVAA JEZI MAALUM LEO IKIWA NI KAMPENI YA KUZUIA UPOFU.

Ili kuamsha na kuhamasisha uelewa wa kampeni: Steven Gerrard (kushoto) and Martin Skrtel (kulia) watakuwa sehemu ya wahusika watakao tinga jezi zenye ujumbe wa kampeni usiku wa leo.
 Kuelekea mchezo wa leo kati ya Man United na Liverpool watavaa jezi maalum zilizoandikwa “Seeing is Believing” (Kuona ni kuamini) ikiwa ni kutoa sapoti ya kuongeza uelewa wa kampeni ya kuzuia upofu na uharibifu wa uwezo wa kuona.
Liverpool wataungana na wadhamini wao Standard Chartered wanafanya hivyo zikiwa zimepita siku 4 tangu kuazimishwa kwa “World Sight Day” ambayo huazimishwa kila mwaka kwa lengo la kuleta ufahamu juu ya upofu na uharibifu wa uwezo wa kuona.
Ni sehemu ya kampeni ambapo wachezaji mmoja mmoja walifunikwa macho na kugusishwa wanyama na wadudu wanao waogopa ambao hawakutaraji kuwagusa maishani kama vile nyoka, kasa, konokono na nge, paka, panya na kadhalika. 
Watoto wenye uono hafifu wamepewa nafasi kubwa kwenye kampeni hiyo na hapa taswira nazo zimehusishwa kama sehemu ya uelimishaji, kuwahamasisha wazazi wawapeleke watoto wao kliniki kuwapima macho na kupewa tiba ili wapate kuona inavyopaswa.
Sakho na kampeni.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ” nikiwa kama mtu ninayevaa miwani ,ninafahamu kuona ni muhimu katika maisha yangu kwa hiyo hili suala ni muhimu sana kwangu.”

Miwani ya Klopp itapigwa mnada baada ya mchezo ili kuchangia pesa katika kampeni hiyo, na jezi za wachezaji za mechi hiyo, pamoja na kitambaa cha unahodha pia vitauzwa kwa ajili ya kuongeza fedha za kusaidia kampeni hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.