ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 24, 2016

JESHI LA POLISI MKOANI PWANI LIMEFANIKIWA KUIKAMATA GARI AINA YA TOYOTA HARRIER ILIYOIBIWA DSM.

Jeshi la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kuikamata gari aina ya Toyota Harrier ilioibwa jana mchana na watu wasiojulikana eneo la mbezi juu jijini Dar es Salaam likiwa na mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu na kisha kutokomea nalo kusikojulikana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Bonaventura Mushongi amesema gari hiyo yenye namba za usajili T 400 DEH mali ya afisa wa jeshi la wananchi Tanzania kapteni Innocent Philipo Dallu limekamatwa majira ya saba kasoro dakika ishini usiku katika kizuia cha polisi kilichowekwa katika barabara ya Bagamoyo- Msata katika kijiji cha Bago kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo likiwa na watu wawili.

Kwa mujibwa wa kamanda Mushongi mara baada ya gari hilo kuzuiwa na askari waliokuwa katika kizuia hicho dereva wa gari hilo alitoroka na kukimbilia porini na kumuacha mwenzake waliyekua naye ambapo kwa sasa jeshi hilo linaendelea na jitihada za kumtafuta.

Amemtaja mtuhumiwa aliyekamatwa akiwa katika gari hilo kuwa Ezekiel Daud mfanya biashara toka mkoani Kilimanjaro.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.