HOTUBA YA MHESHIMIWA JOHN V.K.MONGELLA, MKUU WA MKOA WA MWANZA,WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO MKUUWA KAWAIDA WA ROBO MWAKA WA CHAMA CHAMAJAJI NA MAHAKIMU (JMAT) TAREHE 01 OKTOBA, 2016MWANZA
Mheshimiwa Robert Vicent Makaramba, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mheshimiwa Francis Kishenyi, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Mkoa wa Mwanza (JMAT), Mheshimiwa Bittony Mwakisu, Katibu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Mkoa wa Mwanza (JMAT),
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza,Mheshimiwa Francis Kabwe, Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza,Wajumbe wa Kamati Tendaji wa Chama cha Majaji na Mahakimu Mkoa wa Mwanza (JMAT),
1Waheshimiwa Mahakimu wote wa Mkoa wa Mwanza na Geita, Wanachama wote wa Chama cha Majaji na Mahakimu Mkoa wa Mwanza na Geita (JMAT),Ndugu wageni waalikwa, Wanahabari, mabibi na mabwana.Naomba kwanza nitoe shukrani zangu za dhati
kwako, Mhe.
Jaji Mfawidhi Kanda ya Ziwa, Mhe.Robert Makaramba, akichangia wakati wa maswali na majibu ndani ya mkutano huo. |
Jaji Mfawidhi, kwa kunialika kujakushirikiana nanyi katika mkutano huu muhimu. Nifursa ya pekee kwangu kukutana nanyi, WaheshimiwaMajaji na Mahakimu na wadau wote wa sekta yasheria. Asanteni sana.
Kwa sasa niruhusuni nisimame mbele yenu kwaunyenyekevu mkubwa kwa kazi ambayo nitaifanya hivipundeNimearifiwa kuwa maudhui ya mkutano huu ni kujadilimaadili ya kazi za waheshimiwa majaji na waheshimiwamahakimu kama njia bora ya kuboresha utendaji kaziwa Mahakama na Utendaji haki.
Nafurahi kufahamu kuwa mkutano kama huuunafanyika kila robo mwaka kwa nia ya kujitathmini.Nafahamu kuwa pamoja na mkutano huu, Mahakamahuwa inafanya mikutano mingine kama vile Baraza laWafanyakazi na ya watendaji wa Mahakama.
Mkutano mnaofanyika leo na mingine ya aina yakeimeiwezesha Mahakama kuendelea kujitathminiyenyewe kiutendaji.
Wawasilishaji wa mada wakiongozwa na muongoza mjadala Jaji Rose Ebrahim (katikati) |
Muwasilishaji kutoka NSSF. |
Katubu wa JMAT MWANZA Mhe. BITTONY MWAKISU (kulia) akiongoza sekretarieti katika mkutano huo. pembeni yake ni Mhe DENICE MLASHANI kutoka Sengerema. |
2Nitoe rai kwa mhimili huu kuimarisha utaratibu huukwani ni wa pekee. Kwa taasisi nyeti na muhimu kamaya kwenu kujitathmini ni nyenzo kuu ya kuboreshautendaji.Waheshimiwa Majaji na Mahakimu, Mihimili yote ya dola yaani Serikali, Bunge naMahakama inapata mamlaka yake kutoka kwawananchi kupitia Katiba.
Hivyo siku zote inatarajiwakwamba katika utekelezaji wa majukumu yake mihimilihii itazingatia maslahi ya wananchi, Katiba na sheriaza nchi.
Mahakama, kama zilivyo nguzo nyingine za dola, inawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba inaelekezajuhudi zake zote katika kuwahudumia wananchi kwaufanisi na kwa wakati.
Ninyi mnafahamu wazi kuwahaki ni eneo muhimu la utawala wa sheria, ni eneo
linalogusa uhai na ustawi wa jamii, na ni eneolinalogusa utulivu na utangamano wa Taifa. Hivyoutendaji wa Mahakama una mchango wa pekee katikataifa letu.
Ili kuhakikisha kwamba Mahakama inatimizawajibu huu bila hofu wala huba, katika nchi nyingi, ikiwemo nchi yetu, imewekwa misingi ya kikatiba nakisheria ambayo imezipa Mahakama uhuru mkubwakatika kuendesha shughuli zake ikilinganishwa namihimili mingine.
3Waheshimiwa Majaji na Mahakimu, Dhana ya upekee wa Mahakama inatokana nauhuru unaotolewa ili kuuwezesha mhimili huukutekeleza kazi zake bila kubanwa na mifumo yakawaida ya upimaji inayotumiwa na taasisi nyingine.Ni wazi, hata hivyo, kwamba uhuru huu una mipakayake. Kwani vipo vyombo vya kisheria vya kufuatiliamwenendo na nidhamu ya watoa haki: mahakimu namajaji.
Pamoja na ukweli huu, utaratibu waMahakama kupimwa ni wa aina yake. Ni vigumukwa watu wa kawaida kuujua au kuuona unavyofanyakazi.
Tofauti na nguzo nyingine za dola, imekuwarahisi, kwa mfano, kwa wabunge kupimwa na wapigakura wao kila baada ya kipindi Fulani.
Sina shaka mpango wenu wa kujitathminiutaiwezesha Mahakama kujiweka karibu sana nawananchi na kujua nini matarajio yao, ili nanyi kwaupande wenu muone namna nzuri ya kutekeleza majukumu yenu kama sehemu ya uwajibikaji waMahakama kwa umma. Waheshimiwa Majaji na Mahakimu, Mwanzoni mwa hotuba hii nimezungumzia uhuru waMahakama.
Kama nilivyosema, uhuru waMahakama ni muhimu sana katika upatikanani haki,
kwani Mahakama ambayo siyo huru, haiwezi kutendahaki. Kama ninyi wenyewe wanasheria mnavyosema:haki inatakiwa siyo tu itendeke, bali ionekaneinatendeka.
4Kama kuna wasiwasi wowote ule wa jinsi hakiinavyotolewa, hasa kutokana na tuhuma za kukosauadilifu, basi haki haiwezi kuchukuliwa kama kweliimetendeka. Wajibu wa Mahakama ni kufanya yotemawili: kutenda haki, na kufanya haki ionekaneimetendeka.Ni matumaini yangu kwamba katika mkutano huupia mtaendelea kuyazungumza masuala ya maadilikwa uwazi.
Lakini msiishie hapa, napenda kutoa mwitokwamba masuala ya maadili katika utendaji waMahakama yawe yanaendelea kuwa ajenda ya kudumu.Waheshimiwa Majaji na Mahakimu,Nimefurahishwa na uamuzi wenu wakuwashirikisha katika mkutano huu wadau mbali mbaliwa Mahakama na sekta ya sheria kwa ujumla ambaopia ni wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa.
Waheshimiwa Majaji na Mahakimu,Nina matumaini kuwa mkutano huu utakuwa wamafanikio siyo tu kwa Mahakama bali kwa wananchiwa Mkoa wa Mwanza, Geita na taifa letu kwa ujumla.Nakutakieni majadiliano yenye tija kwenu na kwa nchiyetu.
5Baada ya kusema hayo nafurahi sasa kutamka kuwaMkutano huu Mkuu wa kawaida wa robo Mwaka wa Majaji na Mahakimu wa Mkoa wa Mwanza na Geita umefunguliwa rasmi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.