ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 7, 2016

HAKIELIMU YALAANI KIPIGO KWA MWANFUNZI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage. 
Dar es Salaam. 
Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia masuala ya elimu nchini, Haki Elimu limelaani kitendo cha adhabu ya kikatili iliyotolewa na walimu wa mafunzo kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Mbeya Day, Sebastian Chinguku.
Akizungumza na vyombo vya habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage alisema vitendo hivyo vinachangia kwa kiasi kikubwa watoto wengi hususani wa kike kuacha shule hivyo kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Alisema serikali ihakikishe kuwa miongozo yake ya kusimamia na kuimarisha nidhamu shuleni inazingatiwa na watu wote.

"Serikali inapaswa kuanzisha mifumo rasmi ya kutoa taarifa dhidi ya matukio ya ukatili yanayoendelea katika shule zetu itakayowawezesha wanafunzi na wadau wengine kutoa taarifa mara wanapokutana na matukio ya kikatili kama haya kwa lengo la kuyakomesha," alisema Kalage.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.