ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 20, 2016

GNRC WAHITIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUTOKOMEZA UMASKINI KIPEKEE.

Wanafunzi wa shule ya Msingi  Oysterbay wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baraka Chedego kutoka GNRC -Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu
Wanafunzi wakiwa katika mdahalo.
Vainess Mbaga  (Education Officer) akitoa elimu kwa watoto.
Washiriki wa Mdahalo wakisalimiana na Mama Joyce Mdachi kutoka GNRC na viongozi wengine wa shule.
Mtanange dimbani.
Maufundi zaidi na vyenga.....
Kipyenga kimelia.
Huduma ya kwanza.
Elimu ya Futboli.
Ushirika na ushirikiano.
Mduariko.
Marafiki.
Skul baraza.
Mfano wa vyeti walivyotunukiwa wanafunzi kutoka na ushiriki mzuri wa siku hii ya kipekee.
Kila tarehe 15 Oktoba, Dunia nzima huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umasikini, ambapo mwaka huu  kauli mbiu ya  siku hiyo ilikuwa ni
‘’KUTOKA UDHALILISHAJI NA UTENGWAJI MPAKA USHIRIKISHWAJI ‘’.

Mtandao wa Dini mbalimbali kwaajili ya watoto ulimwenguni  uitwao Global Network of Religion for Children (GNRC-Tanzania) wamefanikiwa kuhitimisha siku hii kwa namna ya pekee kabisa ambapo tangu tarehe 15 Oktoba wamekuwa wakiandaa matukio mbalimbali yaliyolenga kuwajengea uwezo watoto haswa wa Shule za msingi kwa kuandaa mashindano tofautitofauti kama Midahalo na Michezo ikiwa na lengo la  kuwajengea watoto uwezo (capacity building)  na kuwapa elimu ambayo itaweza kuwakomboa katika janga la umasikini . 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.