ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 26, 2016

KESI YA KUPINGA UMEYA KINONDONI YAPANGIWA HAKIMU.

Kesi ya kupinga uchaguzi wa Umeya na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam iliyofunguliwa na Chadema katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepangwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage kwa namba 304 ya 2016.
Katika kesi hiyo Chadema kupitia wakili wake, John Malya wanaiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itengue uchaguzi huo na pia wanaomba mahakama iamuru uchaguzi huo uitishwe upya na walipe gharama za kesi.

Walalamikaji katika kesi hiyo ni Mustafa Abdul Muro na Jumanne Mbunju dhidi ya Benjamin Sitta, Manyama Mangaru, Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Kinondoni, Msimamizi wa mkutano huo na Meya na Naibu Meya wa Kinondoni.

Mwanasheria wa chama hicho, John Malya amesema, wamefika mahakamani hapo ili kueleza walichokifanya walalamikiwa si sahihi na kwamba wamekwenda mahakamani hapo kwa ajili ya kutafuta haki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.