ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 22, 2016

BHUDAGALA - NG'WANAMPELA

Bhudagala ni jina lililo maarufu katika zama za sasa ndani ya kabila la watu wa Sukuma, ukipata nafasi kuingia ndani ya wilaya na vijiji mbalimbali kanda ya ziwa utapata majibu ya hiki ninachokujuza hapa.

Nimewahi kuhudhuria sherehe mbalimbali za wadau kanda ya ziwa ikiwa ni pamoja na matamasha na kupata fursa ya kuzisikia na kushuhudia watu wakizicheza nyimbo za jamaa huyu tena zikiombwa na kurudiwa rudiwa.

Jamaa anajaza show zaidi ya vile unavyodhani tena bila ya promo ya redio wala mitandao.

KISA NA MKASA
Ujumbe unaowasilishwa unaigusa jamii ukielezea maisha halisi ya watu wa kijijini wa hali ya chini na changamoto zao umekuwa kichocheo cha yote hayo, na haiishii hapo lugha nayo imekuwa sababu ya kuusababisha muziki wa jamaa huyu kuvuma sana kwani wengi hasa vijiji vya ndani usukumani hawaijui vyema legha ya kiswahili hivyo kwa mwanamuziki huyu kuimba akitumia lugha mama ya kabila lake imekuwa kichocheo cha kukubalika.

Lakini kingine kikubwa ni uwezo pia katika kuimba na kucheza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.