ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 19, 2016

'YANGA YAINYOA TOTO NYUMBANI' 0-2

Kikosi cha Toto Africans kilichoshuka leo dimbani kukiputa na Yanga dimba la CCM Kirumba Mwanza ambapo Yanga waliibuka wababe kwa ushindi wa 0-2.
Kikosi cha Yanga kilichoshuka leo la CCM Kirumba kukiputa na Toto Africns, Yanga waliibuka wababe kwa ushindi wa 0-2.
Kipa wa Toto Africans David Kissu akianua.
Mshambuliaji wa Yanga Hassan Ramadhan 'Kessy' akimtoka beki wa Toto Africans Salum Abdalah Chuku.
Krosi kuelekea lango la Toto Africans.
Kasi.
Yanga wakicheza kandanda safi walijipatia bao la kuongoza kunako dakika ya 29 mfungaji akiwa Obrey Chirwa aliyefunga kwa kichwa, baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa mshambuliaji wa timu hiyo Donald Ngoma ambapo bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.

Mpira wavuni goli la kwanza la Yanga huku kipa wa Toto Africans David Kissu akiambulia patupu.
Shangwe.
Beki wa Toto Yusuph Mgeta akilalamikia wenzake baada ya kufungwa.


Na Albert Sengo
Timu ya soka ya Dar Young African Leo imefanikiwa kunyakua pointi tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara baada ya kuitandika timu ya Toto affrican ya jijini hapa kwa jumla ya bao 2-0 katika mchezo uliofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na Yanga kwa kiasi kikubwa hasa katika dakika 25 za kipindi cha kwanza, ambapo Toto walichezeshwa nusu uwanja.

Angalau ushindani uliibuka kwa pande zote mbili kwa dakika 15 kabla mwamuzi hajaamua kupuliza kipyenga kuashiria mapumziko, lakini walikuwa ni wana wa Jangwani, Yanga wakicheza kandanda safi walijipatia bao la kuongoza kunako dakika ya 29 mfungaji akiwa Obrey Chirwa aliyefunga kwa kichwa, baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa mshambuliaji wa timu hiyo Donald Ngoma ambapo bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Toto African kulishambulia lango la Yanga lakini hawakupata kitu kwani Yanga nao waliamka na kufanya mashambulizi kadhaa ambapo mnamo dakika ya 55 mchezaji Simona Msuva aliipatia timu yake ya Yanga bao la pili baada ya mchezaji Deus Kaseke kuangushwa ndani ya eneo la 18 handi mchezo huo unamalizika timu ya Yanga inaibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Toto African.

Mara baada ya mchezo huo Kocha mkuu wa timu ya Yanga Mholanzi Hans Van Da Pluijm amesema kuwa malengo yake ilikuwa ni kupata pointi tatu katika mchezo huo “ Tulitegemea upinzani wa hali ya juu ndani ya Toto African na tumeweza kutimiza malengo yetu,tutaendelea kupigana ili tupate pointi katika michezo yetu iliyosalia” alisema

Kwa upande wake Kocha msaidizi wa timu ya Toto African Khalfan Ngassa ambaye hakuwepo kwenye benchi kutokana na kibali chake cha kuifundisha timu hiyo kufika kikomo amesema kuwa ameambiwa dakika za mwisho na anaamini kuwa timu yake imepoteza mchezo huo kutokana nay eye kutoonekana kwenye benchi la timu hiyo “ Nimeambiwa na viongozi kuwa kibali kiliichoombwa na cha mimi kukaa kwenye benchi kilikuwa cha muda mfupi hivyo hilo nalo limechangia timu yangu kupoteza mchezo huo” alisema
Kwa matokeo hayo Toto African sasa imeshuka na kukaa mkiani mwa ligi kuu Tanzania bara baada ya kucheza jumla ya michezo 11 na kujikusanyia pointi 8 pekee huku katika mchezo ujao timu hiyo ikitarajia kucheza na timu ya soka ya Simba kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.