ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 20, 2016

AWAUWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYA NCHA KALI MWANZA.

NA ANNASTAZIA MAGINGA, 
GSENGO BLOG,
Mwanza.

MTU  mmoja alieyefahamika kwa jina la Dema Charles (20) Mkazi wa kata ya Ibungulo Wilayani Magu ameuwawa na wengine wawili kujeruhiwa na watu wasio julikana kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika miili yao.

Tukio hilo limetokea tarehe 18 saa 5 ambapo marehemu aliuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali Shingoni huku Mariamu Lukas (26) alijeruhiwa kwenye mkono na Kipele Makubi (90) ambaye ni baba wa nyumba hiyo alijeruhiwa mgongoni  na kichwani na kwamba wako hospitalini kwa matibabu zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kamanda wa polisi Amed Msangi amesema watu hao ambao hawakufahamika kwa wakati walifika kwenye nyumba hiyo usiku na kuanza kufanya maujai hayo na kwamba upelelezi bado unaendelea.

Kwa mujibu wa kamanda amesema kufuatia upelelezi wa awali imesadikika kuwa ni kisasi ndicho kinalipizwa na watu hao kwani imekuwa ni jaribio la nne wakiwa wanamatafuta mama mwenye nyumba hiyo ambaye hakufahamika jina lake na kwamba siku ya tukio hakuwepo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.