ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 6, 2016

WABONGO NAO MATE YAWATOKA..!! WALITAKA SHINDANO LA MISS MAGEREZA.


👑Pichani mshindi wa kinyang'anyiro hicho👆Mkenya 🔥🔥Huku mfungwa Mtanzania akinyakua nafasi ya pili kwenye kinyang'anyiro cha kusaka Miss Prison nchini humo ..... Sasa wabongo nao mate yawatoka eti - watamani mfumo huo.

Kiu yao ni kuona Mamlaka husika kuona haja ya kuwa na utaratibu kama huo kwa magereza zetu hapa nchini Pia #KAZINANGOMA ya JEMBE FM imezama kwa undani zaidi kujua Mtanzania huyo ana kesi gani, anatoka mkoa gani, na mengineyo.

Tumezungumza na msemaji mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Tz kafunguka zaidi sauti yake inasikika hapo chini.....

Mtanzania anayesadikiwa ni  mfungwa   uko nchini Kenya  ameweza kujishindia nafasi ya pili ya mashindano ya ulimbwende  ya  Langata Miss Prison 2016,   Mashindano hayo  ufanyika kila Mwaka nchini Kenya kwa wafungwa Wanawake ambapo huwa ni Utaratibu wao wa kila Mwaka .

Ata hivyo Mtanzania huyo ambaye jina lake halijaafahamika  vyema  Inasadikiwa ni mwenyeji kutoka mkoani Arusha  ambaye    anayeshikiliwa nchini Kenya  Katika gereza la Langata uku ikisadikiwa anakabiliwa na tuhuma za kukamatwa na dawa za kulenvya nchini humo .
Akizungumza na GSENGO BLOG kupitia Jembe fm, Msemaji wa Jeshi  la Magereza nchini Tanzania Lukas Mboje, amethibitisha kuwepo kwa Mtanzania  huyo aliyeshinda nafasi ya  pili katika mashindano ya Ulimbwende kwa wafungwa wanawake nchini Kenya.

“Wenzetu wa Magereza ya Kenya wanautaratibu huo wa Miss Prison ambao hufanyika kama sehemu ya ya kuwapa Entertainment, lakini pia ni moja ya utekelezaji wa Urekebishaji  kwa Wafungwa waliopo Magerezani, 

BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

Lakini Mashindano kama haya yanawafanya wafungwa wanawake kuwa na wao wana haki sawa kama watu wengine walioko Uraiani ijapokuwa wao wapo magerezani kutokana na ukinzani wa Sheria,alisema Lukas Mboje.

Hata hivyo Msemaji huyo amesema pia Utaratibu kama huu umekuwepo hata kwa wafungwa wa ndani kwetu  Tanzania ,ijapokuwa matukio yao yamekuwa hayarushwi katika vyombo vyetu vya habari kutokana na sheria ya Magereza inayowazuia kuchukua matukio hayo (Prison Act 1967).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.