ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 15, 2016

VISIMA 7 KUPUNGUZA TATIZO LA MAJI KISHAPU

Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya Kishapu Bwana. Stephen M Magoiga akizindua moja kati ya Visima saba.
Afisa Mradi Mwandamizi Mama Tina Mosha Akimtwisha maji Moja ya wanakiji wa IKONDA.
Moja visima vilivyokuwa vikitumiwa na wananchi kabla ya ujenzi wa visima vya kisasa.
Vijana wa Youth CAN wakitoa elimu ya Mazingira, Majina Afya kwa njia ya Nyimbo Kijijini Ikonda.
Vijana wa Youth CAN wakitoa elimu ya Mazingira, Majina Afya kwa njia ya Nyimbo Kijijini Ikonda.
Nizar Selemani Mratibu wa shuguli za vijana katika shirika la NCA na Baraka Chedego ambae ni Mratibu wa Youth CAN wakizungumza jambo wakati wa mkutano na wanakijiji cha Ikonda.
Vikundi Mvalimbali vya sanaa kutoka Kishapu vikitoa burudani wakati wa Mkutano.
Wananchi wa Kishapu wakifatilia mkutano kwa Umakini Mkubwa.
Wananchi wa Kishapu wakifatilia mkutano kwa Umakini Mkubwa.


MSAFARA WA VIJANA WATOA ELMU YA MAZINGIRA NA AFYA KISHAPU
Youth Climate Activist Network (YouthCAN) Tanzania Ni mtandao wa vijana wanaotoka kwenye taasisi za dini mbalimbali wanaofanya shuguli mbalimbali za mazingira na afya kwa ujumla kwa kujitolea chini ya Shirika la Norwegian Church Aid (NCA)
Kuanzia Tarehe 11/9 /2016 vijana hawa walianza masafara wa Kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi. 

Ilikutoa elimu ya Utunzaji wa mazingira, vyanzo vya maji na usafi baada ya kutoa elimu hiyo Halmashauri ya wiliya Kishapu Mkoani Shinyanga wanatarajia kwenda Kutoa elimu hiyo Mkoani Manyara kwenye baadhi ya vijiji vilivyopo Hanang. Hydom na Mbulu.

Licha ya kutoa elimu juu mazingira, Maji ana afya vijana hawa watapata nafasi ya kuzindua baadhi ya Visima vya maji vilivyojengwa na Shirika la Norwegian Church Aid (NCA) kwa kushirikiana na Washirika wake.

Ambapo kwa kuanza wamepata fursa ya kushiriki uzinduzi wa visima 7 vilivyojengwa kwa msaada wa watu wa Norway visima hivyo vitasaidia kutatua tatizo la maji safi na salama katika vijiji vi 3 wiliyani Kishapu ambavyo ni IKONDA A,UBATA na MWAWEJI.


Picha zote na IMANI SELEMANI NSAMILA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.