ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 28, 2016

PICHA RAIS MAGUFULI AZINDUA RASMI NDEGE MBILI ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI KWAAJILI YA ATCL JIJINI DAR LEO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
93.7 JEMBE Fm... SEHEMU YA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI.

"NAOMBA KUZITAJA DHAMBI ZA ATCL :- Ni shirika ambalo lilikuwa likijiendesha bila faida hivyo halikuwa na tija kwa taifa"

"Palikuwa na mafuta hewa:- Kwamba ndege imeondoka leo inaenda Mwanza kumbe ndege ipo hapa hapa na imejazwa mafuta"

"Kwa hiyo tunazungumza wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa, lakini palikuwa na mafuta hewa hapa ATC"

"Paliwahi kupotea zaidi ya shilingi milioni 700 kituo cha Comoro na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na huyu muhusika aliyehusika kupoteza hizo milioni 700 baada ya kustaafu mwezi February ameongezwa muda tena ili aendelee kupoteza tena hizo hela"

"Nikiyataja mengine, ni mengi, ila nimeona niyazungumze haya ili Bodi ya ATCL mjue majukumu kubwa mbele yenu" #JPM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiingia kwenye ndege mojawapo baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoka kwenye ndege mojawapo na kuelekea ingine baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.
PICHA NA IKULU.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.