ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 2, 2016

NEW GENERATION ZANZIBAR, MBASPO MBEYA MABINGWA Airtel Rising Stars.

Nahodha wa timu ya New Generation Amina Hali Abdallah (nyekundu) akikabidhiwa kombe na Afisa Habari wa ZFA Ali Bakari baada ya kuichapa timu ya Women Fighter 2-1 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar Jana 25 Agosti 2016. New Generation ilishinda 2-1.
Wachezaji wa timu ya New Generation wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa baada ya kuifunga Women Fighter 2-1 kwenye fainali za michuano ya Airtel Rising Stars Zanzibar, zilizochezwa kwenye uwanja wa Fuoni Alhamisi 25 Agosti 2016

Naodha wa timu ya Mbaspo Academy Mbeya, Biva Steven akipokea kikombe kutoka kwa mgeni rasmi Katibu Tawala wa mkoa huo Alone Mbinga baada ya timu yake kuifunga Uyole Alois Academy Penati 4-3  katika mchezo wa fainali ya Airtel Rising stars ngazi ya mkoa uli0pigwa katika dimba la uwanja Sokoine juzi.
Wachezaji wa Mbaspo wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe cha ubingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa Mbeya juzi. 

New Generation, Mbaspo mabingwa Airtel Rising Stars
TIMU ya wasichana ya New Generation imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Star, Zanzibar, baada ya kuifunga Women Fighter kwa mabao 2-1 katika fainali iliyochezwa visiwani humo jana.
Mchezo huo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Fuoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar na kuvuta hisia za mashibiki wengi wa soka wanawake na wanaume, hasa kwa vile timu hizo zina upinzani wa jadi.
Mabao ya New Generation yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza ambapo bao la kwanza lilifungwa na Warda Mwinyi katika dakika ya 10 wakati bao la pili lilifungwa mnamo dakika ya 16 wakati bao la kufutia machozi la Women Fighter lilifungwa na Khadija Hassan dakika ya 27.
Akizungumza wakati wa kukabidhi kombe kwa washindi afisa habari wa chama cha soka Zanzibar ZFA Ali Bakari Cheupe kwa niaba ya rais wa chama hicho, aliipongeza kampuni ya Airtel kwa uamuzi wake wa kudhamini michuano hiyo ambayo imeweza kuleta hamasa kubwa kwa wananchi wa Zanzibar.
Alisema kabla ya michuano hiyo Zanzibar ilikuwa nyuma katika soka la wanawake lakini kupata udhamini huo ari imeongezeka zaidi na tayari wanawake wengi wamehamasika kutaka kucheza mpira wa miguu.
Naye Meneja Mauzo wa Airtel Muhidin Mikidad alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia michezo hiyo kadri ya hali itavyokuwa, ambapo amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuwaunga mkono

Jijini Mbeya, timu ya wavulana ya Mbaspo Academy  imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ya kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi baada ya baada ya kuifunga Uyole Alliance 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Mchezo huo uliamuliwa kwa penati kufuatia timu hizo kutoka sare ya kufungana 3-3 katika muda wa kawaida wa dakika 90.

Katika mchezo huo ulipigwa juzi katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ulishuhudia vijana wa Uyole Alliance kutoka nje kidogo ya jiji la Mbeya wakijipatia goli la kuongoza katika dakika ya saba baada ya Daniel Shaban kufunga kwa penati baada mchezaji wa timu hiyo kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

Mbaspo walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha katika dakika ya 20 kupitia kwa Albinus Haule kabla ya Claud Alex wa Uyole Alliance kuandika bao la pili timu yake dakika ya 42.

Mabao mengine kwenye mchezo huo yalipatikana dakika 82 kwa upande wa Mbaspo mfungaji Shadraki Sape,wakati bao la Uyole Alliance lilipatikana dakika ya 88 mfungaji ni Claud Casto.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.