ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 30, 2016

MISS LAKE ZONE 2016 ANYANG'ANYWA GARI LAKE ALILOZAWADIWA. AANGUA KILIO...!!

Gari aliyozawadiwa mshindi wa Miss Lake Zone, ILLUMINATA DOMINICK yakamatwa na kampuni ya ZamZam Motors kutokana na deni la Milioni sita na laki moja.

Makubaliano kati ya ZamZam Motors na kampuni ya Ozona ambae ndie mdhamini mkuu wa Miss Lake Zone 2016, ilikua ni malipo ya awali Milioni tatu na laki tano pesa taslimu na cheki ya pesa yenye thamani ya shilingi milioni sita na laki moja ila akaunti ya fedha ilioandikiwa cheki hiyo haikua na salio lolote.

Hivyo kupelekea kuchukua hatua ya kulikamata gari hilo. Baada ya sakata hilo kufikia hapo Jembe Fm kupitia kipindi chake cha #SPORTRIPOTI KINACHORUKA KILA SIKU ZA SAA 3 KAMILI USIKU HADI 4 KAMILI, KASORO SIKU YA IJUMAA AMBAPO KIPINDI HICHO HURUKA SAA 2 USIKU HADI 3, ILIWASAKA WADAU WOTE ILI KUWEKA MAMBO HADHARANI NA HIKI NDICHO WALICHOSEMA.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Akifanya mahojiano na waandishi wa habari siku alipotwaa taji la Miss Lake Zone 2016 na kukabidhiwa gari hilo. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.