ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 9, 2016

ERIC OMONDI KUWAWEKA KIKAANGONI WAREMBO WA OZONA MISS LAKE ZONE NDANI YA JEMBE FM.

 Mchekeshaji maarufu wa Afrika Mashariki kutoka nchini Kenya Eric Omondi hii leo anatarajiwa kuwaweka kikaangoni warembo wa kinyang'anyiro cha Ozona Miss Lake Zone 2016 ambao wanamaliza kambi yao usiku wa kuamkia kesho na hiyo kesho kutinga kwenye jukwaa moja kushindana katika fainali kumsaka nani atakaye litwaa taji hilo ambalo limekuwa gumzo si Kanda ya Ziwa pekee bali pia limesisimua wana wa Taifa zima.

Kwa mujibu wa GSengo ambaye pia ni mmoja wa watangazaji watatu wa kipindi cha Kazi na Ngoma kinachoruka Radio Jembe Fm 93.7 Mwanza saa 5 asubuhi hadi saa 7 mchana amesema Eric Omondi  atakuwa mchekeshaji wa kwanza kuwa mtangazaji wa kwanza  kipindi cha Kazi na Ngoma akiendesha mahijano kama main prizenta yaani mtangazaji mwongozaji namba moja akisimama line one kuhoji kila atakachohitaji ufafanuzi toka kwa wanyange hao ikiwa ni sanjari na kupima IQ zao na kupokea simu na sms za wasikilizaji watakao kuwa wakifuatilia kipindi.
 Watangazaji wengine wa Kazi na Ngoma ni Mansour Jumanne na Mwaka Mzima huku mashine za burudani zinazokamilisha neno Ngoma zikipewa shida na Dj Scorpion toka JEMBE DJz.
Hapa Eric alikuwa akitafakari jina 'JEMBE' Kicheko kikachomoza
 'Ujumbe Kicheko muhimu kwa afya' 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.