WATUMISHI wa umma Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wametkakiwa kuachana na vitendo vya kuwa na tamaa, ya kupokea rusha au kutoa kwa lengo la kuweza kuuza viwanja kiholela bila ya kuzingatia sheria na utaratibu kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha kuwepo migogoro ya ardhi ya mara kwa mara kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Erica Yegella kikao maalumu cha mafunzo ya kazi kilichoandaliwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuweza kutimiza majukumu yao ipasavyo wajumbe wa mabaraza ya ardhi na nyumba ngazi ya kata zilizopo katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Yegella alisema kwamba watendaji wa ngazi zote kwa kushirikiana na wajumbe wa mabaraza wanapaswa kuitambua vizuri sheria ya ardhi ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua migogoro ambayo imedumu kwa kipindi cha muda mrefu ikiwa sambamaba na kutenda haki bila ya kuwa na upendeleo wowote ili kuepukana na vurugu ambazo zinapelekea uvunjifu wa amani.
Aidha alisema kwamba ana imani baada ya watendaji hao kupatiwa mafunzo hayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kutatua migogoro ya ardhi ambayo wakati mwingine inapelekea kuwepo kwa vurugu kutokana na kugombania viwanja.
Naye Afisa kutoka tume ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya Mashariki Seleman Shaban amewataka watendaji nawatumishi wa umma kuhakikisha wanazingatia maadili na taraibu zote za kazi zao ili kuepukana na suala la kutoa au kupokea rushwa kwani ni kinyume kabisa na sheria za nchi.
Jerome Njiwa ni Mwenyekiti wa baraza la ardhi katika Wilaya ya Kibaha ambaye alihudhuria katika kikao hicho na hapa anafafanua zaidi kuhusina na migogoro mingi ambayo imekuwa ikijitokeza katika mabaraza ya ardhi ya kata na nyumba kutokana na kutozifahamu sheria vizuri.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata na nyumba warioshiriki katika mafunzo hayo akiwemo Mwinyikondo Asia, Mariamu Swala pamoja na Hassan Ally wamesema kwamba walikuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi katika ufanya maamuzi kutokana na kutozijua vizuri sheria za ardhi.
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wamewashirikisha wajumbe mbali mbali kutoka katika mabaraza ya ardhi ya kata zilizopo katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kupunguza kero na migogoro ya aradhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara na kusababisha vurugu kwa wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.